Samson Daudi (26) Mkazi wa Kijiji cha Mutuka Wilayani Babati Mkoa wa Manyara anatuhumiwa kumuua Peter Buu(48) ambaye alimtuhumu kumroga ili nyumba yake isiishe.
Tukio hilo limetokea Septemba 5, 2021 ambapo Mtuhumiwa alikwenda shambani kwa marehemu ndipo mzozo ulitokea, akamshambulia mara tatu shingoni kwa panga na kufa palepale.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Grafton Mushi amewataka Wananchi kutafuta suluhu kwa kufikiria njia sahihi na siyo kwenda kwa Waganga wa Kienyeji ambao watawapotosha.
Social Plugin