Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALAMA ZA ASILI ZATAJWA KUWA CHANGAMOTO KWA WALEMAVU WA KUSIKIA

Wanafunzi  wakiwa darasani

Na Frankius Cleophace Rorya.

Alama za asili zinazotumiwa na wazazi na walezi pamoja na jamii inayozunguka watoto wenye umri wa miaka sifuri mpaka nane wilayani Rorya Mkoani Mara zinatajwa kuwa changamoto pindi walimu wanapofundisha mashuleni kwa kutumia lugha za kitalaamu.

Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu kata ya Koryo wilayani Rorya Malaika Gabriel wakati akizungumzia siku ya Lugha ya alama kimataifa ambayo hufanyika Septemba 23 kila mwaka.

Malaika alisema kuwa wanafunzi wadogo chini ya miaka Mitanoa ambao wanaanza darasa la awali katika shule ya kutoa elimu maalumu Utegi iliyopo wilayani Rorya Mkoani Mara wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya uelewa wakati wa kufundishwa Lugha za kitalaamu kwa sababu ya kukariri lugha za asili ambazo jamii inawafundisha tangu wanapozaliwa mpaka kufikia umri wa kwenda shule.

“Mimi ni Afisa elimu kata ya Koryo pia ni mwalimu wa Lugha za alama katika shule ya msingi Utegi tunapata changamoto kubwa katika ufundishaji kwa wanafunzi hususani wadogo kwa sababu wao wamekalili lugha za asili sasa wanapoletwa shuleni hapa tunalazimika kutumia Lugha za kitaluma jambo ambalo linawapa changamoto kubwa ,unaweza kukuta wanakubali tu lakini hawaelewi kile tunachofundisha nasisitiza wazazi na walezi kuwaleta mapema watoto wenye ulemavu wa kusikia ili kuwajengea misingi bora mapema” alisema Gabriel.

Pia Gabril alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa majengo kwani wanafunzi wote takribani 51 wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwemo wa Kutosikia, walemavu wa vioungo, walemavu wa kutoona darasa la awali mpaka la saba wote wanatumia chumba kimoja katika ufunindishaji na ujifunzaji jambo ambalo linaweza kuchangia taaluma kushuka.

“Tunaomba serikali kwa kushirikiana na wadau kutatua changamoto ya miundombinu ya ujifunzaji ili kuwasaidia wanafunzi wetu wanaopata elimu maalumu kwa sababu mazingira siyo rafiki” alisema Malaika.

Vile vile Afisa elimu alisema kuwa bado kuna changamoto ya uhaba wa walimu kwani walimu waliopo mpaka sasa ni walimu watano tu wanaofundisha wanafunzi 51 kwa kutumia chumba hicho kimoja ambapo hupishanisha wanafunzi hao iliwengine waendelee kupata elimu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka alisema kuwa katika kutatua changamoto zinazokabili shule ya msingiu Utegi kitengo cha Elimu Maalumu tayari wamepata mdau atakayejenga vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu ya vioo ili kusaidia kutatua changamoto.

Pia mkuu wa wilaya aliongeza kuwa tayari amemwagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya kuhakikisha wanatatua pia changamoto ya upungufu wa watendaji katika shule hiyo.

“Nimepata mdau tayari ni barua inayozungumzia masuala la bajeti nimeishaipata na ujenzi huo utaanza mwaka huu wala hautachelewa na shule hiyo ni kata ya shule ambayo tumeiweka kwenye mkakati wa kukarabati miundombinu yake ili wanfunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma pale waweze kuwa na mazingira rafiki” alisema mkuu wa wilaya Chikoka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com