Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za mauaji ya mkewe na watoto wawili wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa kichwani na mchi wa kutwangia kisha miili yao kutelekezwa ndani ya nyumba waliokuwa wakiishi huko katika Kijiji cha Mkolye Wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Kamanda wa Polisi mkoa waTabora, ACP Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa moja usiku ikiwa ni mfululizo wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia ambayo yameendelea kutokea wiki hii huko mkoani Tabora.
Social Plugin