Na Magrethy Katengu - Dar es Salaam
Licha ya elimu inayotolewa juu ya kukata bima lakini bado kundi kubwa la watu linakabiliwa na changamoto ya kuamini kuwa bima ni ya watu wa kipato fulani hali hiyo inachangiwa na kukosa taarifa muhimu.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ankra Insurance Agency Co. Ltd Brito Burure amesema Watanzania wengi hukata bima zilizo na msukumo wa kisheria sio kwa lengo la kulinda vitu vyao vya thamani bali hukata bima kukwepa adhabu za mkono wa sheria.
''Wamiliki wa vyombo vya moto ikiwemo pikipiki,gari,bajaji hukata bima mapema kabla ya kuanza kutumia chombo cha moto kukwepa adhabu kwani alikutwa anatumia chombo hicho huchukuliwa hatua kali hivyo bima hizo kutokana na kuwekwa sheria ndizo zinaongoza kwa kuwa na kundi kubwa",alisema Buriro.
Hata hivyo amesema mojawapo ya athari ya ombwe ni watu kuchelewa kutafuta bima hadi pale wanapofikiwa na majanga muda ambao si sahihi kukata bima na asilimia kubwa ni bima ya afya mtu akipata mgonjwa kwenye familia yake hukumbuka kutafuta bima muda ambao sio sahihi.
Sanjari na hayo amesema kampuni ya Ankra imekuja na suluhisho kutoa elimu na kutoa ajira kwa vijana kuanzia umri wa miaka 18- kuwa Mabalozi wa kampuni hiyo ya bima kutangaza popote Tanzania kwa kutoa elimu kwa Jamii iliyomzunguka umuhimu wa kukata bima mbalimbali ikiwemo ya mazao,nyumba,biashara
Social Plugin