DAKTARI mmoja katika eneo la Nakuru nchini Kenya anadaiwa kuwaua wanawe wawili wenye umri wa miaka mitano na mitatu kwa kuwachoma sindano.
Dk. James Gakara alikutwa amelala kando ya wanawe akiwa amepoteza fahamu katika kisa ambacho anashukiwa kutekeleza mauaji na kujaribu kujiua.
Dk. Gakara ambaye alikimbizwa ili kupata matibabu katika Hospitali ya Nakuru Level Five, naye aliaga dunia Jumatano, Septemba 22, 2021.
Kulingana na ripoti ya upasuaji wa maiti, Gakara alimeza kemikali isiyojulikana ambayo huenda ilisababisha kifo chake.
Daktari aliyeendesha zoezi la upasuaji kubaini chanzo chake, Dkt. Titus Ngulungu amesema kwamba huenda marehemu alikunywa dawa.
Social Plugin