Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele
Na Frankius Cleophace - Tarime.
Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele amesisitiza elimu kwa watoto wadogo ili kujengewa misingi bora ya kujua na kutambua vivutio vilivyopo katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mkuu wa wilaya alisema hayo wakati akifanya mahojiano kuhusu siku ya Utaliii duniani ambayo huadhimishwa Septemba 27 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu inasema kuwa Utalii kwa maendeleo Jumuishi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa walimu hawana budi kuendelea kutoa elimu juu ya umhimu na faida za mbuga kwa wanafunzi hususani wale wadogo kuanzia darasa la awali ambao wengi wao wako chini ya miaka mitano ili kuwajengwa kisaikolojia nakuendelea kuyaishi yale watakayo yaona baada ya kutembelea mbuga hizo.
“Mfano kama sisi hapa Tarime kuna Mbuga ya Ramai haijatangazwa sana sasa wanafunzi wakipatiwa elimu na kutembelea hifadhi hzo wataenda kudai kwa wazazi na wazazi wataweza kuwalipia kiasi kidogo cha fedha wanafunzi watatembelea hiyo mbuga wakirudi watasimulia wenzao na wao pia wataenda kudai hivyo tutaweza kujenga kizazi kinachojua vivutio vya hifadhi pia hata wazazi na watu wazima wajenge tabia za kutembelea hifadhi za taifa”, alisema Dc Michael.
Vilevile Mkuu wa wilaya aliongeza kuwa uongozi wa Hifadhi ya Serengeti hauna budi kutoa elimu juu ya faida za uifadhi katika shule za msingi na sekondari jambo ambalo pia linaweza kupunguza Ujangiri ambao umekuwa ukifanyika.
“Nadhani elimu ikitolewa kwa watoto wadogo wa shule za msingi na sekondari watakuwa watu wazima wakijua umhumu wa vivutio vya nchi sidhani kama watajiusisha na suala la ujangiri hivyo suala hilo ni la muhimu sana”, alisema mkuu wa wilaya Tarime.
Vilevile Mkuu wa wilaya alisisitiza wadau wa utalii kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uwekezaji katika hifadhi ya Serengeti kupitia lango la Ramai lilipo upande wa Tarime Mkoani Mara.
“Hebu angalia wenzetu wa Arusha wamejenga makumbusho kwa ajili ya kuifadhi vitu vya kale sasa huku watu wakiwekeza watalii watajitokeza kwa wingi ili kujua kabira la kikurya lilitokana na nini na mambo mengine pia serikali itapata kipato” aliongeza kusema Mkuu wa wilaya Tarime.
Nao baaadhi ya wazazi na walezi wakitoa maoni yao walidai kuwa elimu ianze kutolewa katika shule za msingi na sekondari kuhusu umhimu wa uhifdhai ja jamii iwe mstari wa mbele kupeleka watoto waoo ili kujifunzi utalii.