Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja.akizungumza kwenye mkutano wa 45 wa Mwaka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mbulu uliofanyika wilayani hapo jana. Katikati (mwenye barakoa nyeusi) ni Baba Askofu Michael Adam wa Dayosisi ya Mara.
Baba Askofu Nicolaus Nzangazelu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Mbulu akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja. |
Na Mwandishi Wetu, Hanang.
MKUU wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja amewaomba viongozi wa dini wilayani hapa kuendelea kusimamia malezi na makuzi ya vijana ili kuwa na Taifa lenye hofu ya Mungu, uadilifu na uzalendo.
Mayanja Amametoa ombi hilo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa 45 wa Mwaka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mbulu uliofanyika wilayani hapo jana.
Mayanja alitumia nafasi hiyo kulishukuru kanisa hilo kwa kuunga jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa huduma nzuri kwa jamii.
"Niwapongeze kwa shughuli mbalimbali mnazozitoa kwa wananchi hasa katika sekta ya Afya na Elimu kwani mnaunga jitihada za Selikali kwa vitendo". alisema Mayanja.
Aidha amelihakikishia kanisa hilo kuwa Serikali wilayani humo itaendele kutoa ushirikiano kwa Dayosisi hiyo ili kufikia malengo yao ya kukuza uchumi na utoaji wa huduma za kiroho.
Baba Askofu Nicolaus Nzangazelu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Mbulu amemshukuru mkuu wa wilaya hiyo kwa kushiriki katika mkutano huo na ameahidi kushirikiana na Selikali katika kuimairisha huduma za jamii.
Mkutano huo uliongozwa na Baba Askofu Nzangazelu na kusimamiwa na Baba Askofu Michael Adam wa Dayosisi ya Mara na kuhudhuriwa na watumishi wa Mungu zaidi ya 300 kutoka Wilaya za Mbulu, Hanang, Babati Vijijjni na wilaya za jirani.
Social Plugin