Na Marco Maduhu, Shinyanga
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amewaonya wazazi wilayani Shinyanga, kuacha tabia ya kuwapeleka watoto wenye utapiamlo kwenda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji kwani hawana uwezo wa kutoa tiba hiyo, na wanapozidiwa ndipo hukimbilia hospitali huku watoto wakiwa tayari katika hali mbaya.
Mboneko amebainisha hayo leo, alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha Afya cha Bugisi kilichopo Didia wilayani Shinyanga, na kuhamasisha akina mama wenye watoto walio na utapiamlo, ambao wanapatiwa matibabu kwenye kituo hicho, kuzingatia lishe bora kwa watoto, pamoja na kuwanyonyesha maziwa ya kutosha.
Alisema baadhi ya wananchi wilayani humo, wakiwemo akina mama wenye watoto walio na utapiamlo, wamekuwa na tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kwenda kupatiwa matibabu, badala ya kwenda Hospitali kwenye huduma sahihi, na wanapozidiwa ndipo hukimbilia hospitali.
“Nimefanya ziara kwenye kituo hiki cha Afya Bugisi, nimepewa taarifa kuwa watoto wengi wenye utapiamlo ambao hufika hapa kupatiwa matibabu, wazazi wao huanzia kwanza kwa waganga wa kienyeji kutibiwa, na inaposhindikana ndipo wanawaleta hapa wakiwa tayari na hali mbaya,”alisema Mboneko.
“Natoa wito kwa wananchi wote, acheni tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kupatiwa matibabu, na msiwapeleke huko watoto wenu wenye utapiamlo, bali njooni kwenye huduma za afya mpate tiba sahihi na kuokoa afya zenu na watoto,”aliongeza.
Aidha aliwataka pia akina mama kuzingatia suala la lishe bora kwa watoto wao, na kuwanyonyesha maziwa ya mama ya kutosha, pamoja na wenyewe kula vyakula bora ili wapate maziwa mengi, hali ambayo itawaepusha watoto kupata utapiamlo.
Naye, Dkt. wa kituo hicho cha Afya Bugisi Zacharia Msumari, ambaye anahusika na masuala ya Lishe kwenye kituo hicho, alisema ndani ya miezi sita kuanzia Februari hadi Agosti mwaka huu, walipokea watoto wenye utapiamlo 73, ambapo wengi walianzia kwa waganga wa kienyeji kupatiwa matibabu.
Alisema watoto hao wengine walifika hawana fahamu kabisa, pamoja na kuvimba mwili mzima, na wakawapatia matibabu, ambapo mpaka sasa wameshabaki na watoto wanne ambao ndiyo wanaendelea kutibiwa, huku wengine wakiruhusiwa kwenda nyumbani.
Nao baadhi ya akina mama wenye watoto walio na Utapiamlo akiwamo Yunis Joseph kutoka Lyabukande wilayani Shinyanga, alisema mtoto wake alimfikisha hospitalini hapo kutoka kwa waganga wa kienyeji akiwa hali mbaya, lakini kwa sasa ana afya njema.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia akiwa katika kituo cha Afya Bugisi ambacho kipo chini ya Kanisa la Katoliki Dayosisi ya Shinyanga, kushoto ni Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Kathleen Costigan.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia ,akiwa kwenye Wodi ya watoto wenye Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ,akiwa kwenye Wodi ya watoto wenye Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa kwenye Wodi ya watoto wenye Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia ,akiwa kwenye Wodi ya watoto wenye Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi, kushoto ni Daktari wa kituo hicho Zacharia Msumari akimweleza Mkuu wa wilaya kuwa watoto wengi wenye Utapiamlo ambao wanafika kupatiwa matibabu Hospitalini hapo huanzia kwanza kwa Waganga wa Kienyeji.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia ,akiwa kwenye Wodi ya watoto wenye Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi, kushoto ni Daktari wa kituo hicho Zacharia Msumari akimweleza Mkuu wa wilaya namna wanavyowapatia matibabu watoto wenye Utapiamlo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akiwa kwenye Wodi ya Wazazi na kuwataka akina mama kunyonyesha watoto maziwa ya kutosha, pamoja na wao kuzingatia lishe bora.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akiwa kwenye Wodi ya Wazazi na kuwataka akina mama kunyonyesha watoto maziwa ya kutosha, pamoja na wao kuzingatia lishe bora.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akiwa kwenye Wodi ya Wazazi na kuwataka akina mama kunyonyesha watoto maziwa ya kutosha, pamoja na wao kuzingatia lishe bora.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisalimia Wagonjwa.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisalimia Wagonjwa.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiangalia vifaa Tiba, katika kituo cha Afya Bugisi.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiangalia vifaa Tiba, katika kituo cha Afya Bugisi.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiangalia vifaa Tiba, katika kituo cha Afya Bugisi.
Muonekano wa vifaa Tiba.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo hicho cha Afya Bugisi Dk, Kathleen Costigani namna wanavyo boresha kununua vifaa Tiba.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa kwenye chumba cha Maabara, kushoto ni Mtaalam wa Maabara katika kituo cha Afya Bugisi Elia Daudi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa katika Bohari ya Dawa katika kituo cha Afya Bugisi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipima Presha katika kituo cha Afya Bugisi, mara baada ya kuwasili kwenye kituo hicho.
Na Marco Maduhu- Shinyanga
Na Marco Maduhu- Shinyanga