Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ameomba viongozi na wadau mbambali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuendelea kutoa ushirikiano wa kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ya kazi.
Mboneko ametoa ombi hilo leo katika kikao kazi kwa ajili ya Mradi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na Shirika la The Voice of Marginalized Community(TVMC) chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society (FCS) kwenye kata saba za halmashauri hiyo ambazo ni Usanda,Samuye,Didia,Masengwa,Tinde,Nsalala na Ilola.
Kikao hicho kimehusisha Maafisa watendaji kata,maafisa elimu,maafisa maendeleo ya jamii,maafisa ustawi wa jamii, bodaboda, wakuu wa vituo vya polisi, mahakimu kutoka kata hizo na maafisa kutoka dawati la jinsia polisi wilaya ya Shinyanga.
Mboneko ameliomba shirika hilo la TVMC kwa kushirikiana na
viongozi kutoka kata zilizokutana katika hicho kuwa wakutane na viongozi wa
dini kwa kuwa wao kila wiki wanakutana na waumini huko misikitini na makanisani
ili wafikishe ujumbe wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii pamoja
na kuwashirikisha sungusungu kwa kuwa wao wanashirikiana na jeshi la polisi
kwenye masuala ya ulinzi na usalama.
Naye Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi mkoa wa Shinyanga Analyse Disdory Kaika amesema changamoto wanazokutana nazo kwenye masuala ya ukatili wa kijinsia ni katika ukamataji,upelelezi na ushahidi, amesema katika ukamataji wanatambua sheria zinaruhusu mtu yeyote kukamata lakini changamoto inakuja pale ambapo wanapoenda kukamata pale kosa halijakamilika,katika upelelezi changamoto ni pale mashahidi wanakataa kutoa ushahidi kwa sababu ya hofu kwenye jamii zao kuwa itawachukuliaje na kwa ushahidi madhura wengi wanakengeuka na kupoteza ushahidi kwa kuwa wanakaa na watuhumiwa eneo moja hivyo kumshawishi mhanga akanushe mwishowe kesi inaishia hapo,hivyo ameomba pale upelelezi unapokamilika wahanga wapate sehemu ya kumtunza ili asipoteze ushahidi.
aidha kikao hicho cha mradi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichoanza jana na kufunguliwa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya shinyanga Nice Munissy leo kimefungwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mhe. Jasinta Mboneko kwa makubaliano ya kuendelea kutoa elimu katika jamii hizo hususani kwa wazazi,watoto na waendesha pikipiki za biashara maarufu kama bodaboda ili jamii ielimike na kuachana na vitendo hivyo ambavyo ni hatari kwa maisha ya binadamu.
Social Plugin