Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Nice Munissy
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Bw. Musa Ngangala
Na Josephine Charles - Shinyanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Nice Munissy amezitaka Asasi za Kiraia kuwashirikisha Vijana wanaendesha Pikipiki za biashara maarufu kama Bodaboda kwa kuhusishwa zaidi kwenye maeneo yao kupewa elimu za kupinga Ukatili wa Kijinsia dhidi ya watoto na Wanawake kwa kuwa moja kati ya vyanzo vya ukatili kwa watoto ni waendesha bodaboda.
Munissy ametoa rai hiyo leo Mjini Shinyanga katika Kikao kazi kwa ajili ya Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia unaotekelezwa na Shirika la The Voice of Marginalized Community(TVMC) chini ya Ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) kwenye kata Saba ambazo Samuye,Usanda,Didia,Masengwa,Tinde,Nsalala na Ilola za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kikao hichho kimehusisha Watendaji kata,Maafisa elimu, Maafisa Maendeleo ya Jamii,Wakuu wa Vituo vya Polisi,Bodaboda,Mahakimu,Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka kata husika na Maafisa kutoka Dawati la jinsia Polisi Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza katika Kikao hicho Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Bw. Musa Ngangala amesema lengo la kukutana na Wawakilishi kutoka katika kata hizo ni kuangalia namna gani zinafanya kazi hizo Sheria ndogondogo ambazo ziliundwa 2017 na mpaka kufikia sasa na kuangalia namna gani watazimbaza kwa Jamii iweze kujua kwamba kuna Sheria hizo pamoja na kutengeneza Mpango kazi wa pamoja katika maeneo hayo ili kupinga Ukatili kwa wanawake na watoto kwa kutumia Kamati za Ulinzi na Usalama wa Mtoto.
Kwa Upande wao Washiriki wa Kikao hicho wamesema vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kuisha ni ngumu kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii ikiwemo elimu ndogo kwa Wazazi,Malezi hafifu yasiyo na msingi mzuri kwa watoto hususani mila potofu na kandamizi.
Aidha Mkutano huo umefunguliwa leo Septemba 2, 2021 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Nice Munissy na unatarajiwa kufungwa hapo kesho Septemba 3, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko.