Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. DOROTHY GWAJIMA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA DONALD WRIGHT


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima amekutana na barozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Donald Wright aliyeambatana na mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Mwakilishi kutoka Wizara ya afya, na mratibu kutoka shirika lisilo la kiserikali la USAIDS.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo jijini Dar es Salaam , wamekubaliana kwa pamoja kuimarisha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona UVIKO-19 kupitia afua ya chanjo na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI nchini Tanzania

Bwana Donald Wright amepongeza juhudi zinazoendelea nchini Tanzania kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto huku akishauri serikali kuongeza afua ya utoaji elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujitokeza kupatiwa chanjo ili kukabiliana na UVIKO-19 hapa nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com