DKT. TAX : MASUALA YA ULINZI NA SUALA HAYAWEZI KUTENGANISHWA NA MASUALA YA KIDIPLOMASIA


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax

 Na Magrethy Katengu -Dar es salaam

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema serikali itahakikisha inatoa fursa ya mafunzo  ya diplomasia ya mara kwa mara kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu  ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama ili kuimarisha maarifa ya wajumbe juu ya masuala mbalimbali ikiwemo uchumi.

Dkt. Tax ameyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya Wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ambapo amesema Ulinzi na Usalama hayawezi kutenganishwa na masuala ya kidiplomasia kwa kuwa ndiyo maslahi ya taifa.

Ameongeza kuwa Kamati inalo jukumu la kuhimiza matumizi mazuri ya mitandao na nyenzo nyingine za teknolojia kwa kuwa teknolojia isipotumika vyema itahatarisha usalama wa wa taifa. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amesema mafunzo hayo yamelenga kusaidia kuwajengea uzoefu katika masuala ya kidiplomasia ya uchumi, maslai ya Taifa, uchumi wa blue, na uhifadhi wa nyaraka za kibalozi. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Musa Hassan Zungu amesema taifa haliwezi kukwepa kushirikiana na wawekezaji wa nje kwani kuna miradi mikubwa inayohitaji utekelezaji wa baraka kwa kushirikiana nao itasaidia kupata teknolojia mpya na ubunifu. 

"Uchumi imara unahitaji mabadiliko ya kidiplomasia  hivyo watanzania tusiogope miradi mikubwa ambayo ndiyo chachu ya mabadiliko ya Taifa letu",amesema.

Aidha ameishukuru Wizara hiyo  kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani itasaidia wawapo katika majukumu yao kutetea maslahi  mapana  ya taifa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post