Shirikisho la mpira wa miguu Kenya (FKF) limefuta kazi kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Harambee Stars Jacob Mulee maarafu Ghost.
Cha kushangaza ni kuwa, FKF imefanya uamuzi huo ikiwa ni wiki tatu tu kabla ya mchezo wa Kenya dhidi ya Mali wa kufuzu kushiriki kombe la dunia uliopangwa kufanyika octoba 6 mwaka huu nchini Morocco.
Katika toleo kwa waandishi wa habari, FKF walisema,
“Kocha mkuu wa Harambee Stars Jocob Mulee na msaidizi wake Twahir Muhiddin na kocha wa walindamlango Haggai Azamde wamekubaliana kuondoka”.
Toleo hilo liliongeza na kusema pia, “Wasaidizi wa makocha Ken Odhiambo na William Muluya watabaki kufanya kazi katika benchi la ufundi wakati Kenya ikijiandaa kuminyana na Mali ili kufuzu kushiriki kombe la dunia 2022”.