Je, wewe huwa unapenda kuoga au hupendi kuoga. Kama hupendi kuoga basi nadhani leo utafarijika baada ya kufahamu kuwa yupo mtu asiyependa kuoga kuliko wewe.
Unasema hupendi kuoga lakini huwezi kupitisha wiki bila kuoga, acha kutudanganya wewe unapenda kuoga. Kama hupendi kuoga kweli unaonaje miezi au miaka kadhaa ikapita bila ya mwili wako kugusa maji? Usijali hutakufa.
Yupo mtu ambaye hajaoga kwa miongo kadhaa lakini bado anaishi, yaani tunaweza kusema kwamba yeye ni mchafu kuliko uchafu wenyewe, lakini hilo kwake halimsumbui na huyu si mwingine bali ni mzee ajulikanaye kama Amou Haji.
Haji anaogopa maji, kwa hivyo anachukia kuoga, anaamini ataugua ikiwa ataoga na hii imemzuia kuoga kwa zaidi ya miongo sita.
Amou Haji, raia wa Irani mwenye umri wa miaka 83 ametajwa kama mtu mchafu zaidi ulimwenguni kwani hajaoga katika kipindi cha miaka 65.
Maisha katika jangwa la Irani, na nyama ya nungu nungu iliyooza ikiwa kama chakula chake akipendacho, ndio amezoea. Maisha yake ni uchafu kuanzia anachokula anapoishi na hata mwili wake binafsi.
Ili kuwa na afya hunywa lita tano za maji kutoka kwenye kopo la mafuta lenye kutu kila siku. Pia anapenda kuvuta sigara lakini mtindo wake wa kuvuta sigara unajumuisha kuvuta kinyesi kikavu cha ng’ombe badala ya tumbaku lo! Hutatamani kuwa karibu naye.
Wenyeji wanaamini kuwa moyo uliovunjika ndio sababu Amou Haji alichagua mtindo huu wa maisha. Lakini, bado hajakata tamaa ya kupata upendo.
Haji hana nyumba, anazurura karibu na kijiji kilichotengwa cha Dejgah katika mkoa wa Kusini mwa Irani wa Fars na anaishi kwenye mashimo yaliyotengenezwa jangwani nje ya kijiji. Ingawa wanakijiji walimjengea kibanda lakini alichagua kutoishi hapo.
Amekuwa na rangi inayotaka kufanana na ardhi inayomzunguka na anajichanganya kabisa na mazingira yake. Wenyeji wanasema mara nyingi huwa wanamfanisha na mwamba wakati anapokuwa ametulia kimya. Haji hajali raha za ulimwengu na anaridhika kuishi maisha ya uchafu na ya kuhamahama.
Social Plugin