Ingawa wengi wetu tumeshikamana na simu zetu, tunajua machache kuhusu ukweli wa matumizi yake ,athari na mambo mengi tu .
Zifahamu dhana 6 zinazoshikiliwa na wengi juu ya simu za mkononi ambazo sio kweli.
1. Kuchaji betri yako usiku mzima kutaharibu Simu Yako
Simu za kisasa za mkononi huitwa "smart" kwa sababu maalum . Kwa kweli, vifaa vya leo ni stadi kwa njia hiyo kwa sababu vinajua wakati wa kuacha kuchaji - na vitaacha moja kwa moja vinapohitajika.
Kwa hivyo, ingawa ni kweli kwamba miaka michache iliyopita kuchaji simu yako kuliharibu betri, leo - ilimradi utumie chaja rasmi - simu yako haitaharibika hata ukichaji usiku kucha.
Inafaa kukumbukwa kuwa betri zote za simu za rununu ziko katika hali ya kuoza kila wakati - kwa hivyo hakuna itakayodumu milele.
Walakini, kuchaji simu yako usiku mzima hakutaongeza uharibifu wa betri yako.
2. Megapixels Zaidi ni sawaia na Picha yenye ubora wa juu
Megapikseli ni nini? Ni saizi milioni moja za pikseli. Kwa hivyo, kamera yenye megapikseli 12 inaweza kunasa picha iliyoundwa na pikseli milioni 12.
Watu wengi - pamoja na watengezaji wa simu za smartphone - huzungumzia megapixels kama kiashiria cha msingi cha kamera nzuri. Walakini, siku hizi, ubora wa picha ni muhimu zaidi.
Kwa hivyo yawezekana kwa kamera ya megapikseli 12 zenye ubora wa juu ikachukua picha nzuri kuliko kamera ya megapixel 15 zenye ubora wa chini.
Kwa hivyo, wakati mwingine unaponunua simu, kumbuka, megapixels zaidi haimaanishi picha bora.
3. Wifi -huduma ya bure ya intaneti ni salama
Kwa wengi wetu, Wi-Fi ya bure inaweza kuvutia sana - haswa wakati tunasafiri au nje ya mtandao wetu wa kawaida.
Lakini usichojua ni kwamba mitandao ya bure ya Wi-Fi kawaida huwa wazi na, kwa hivyo, ni hatari kwa mashambulio ya wadukuzi.
Wadukuzi wanaweza kubadilisha ama kuingilia mawasiliano kati ya pande mbili ambazo zinaamini zinawasiliana. Sio jambo zuri .
Kwa sababu ya hii, ni wazo zuri kuepukana na Wi-Fi - za umma .
Wifi hizo hazihitaji uthibitisho wa kuanzisha unganisho la mtandao, na kuzifanya kuwa bora kwa wadukuzi wanaotafuta kupata ufikiaji wa vifaa visivyo salama kwa kutumia mtandao huo.
Ikiwa lazima utumie Wi-Fi ya umma, kila wakati tumia Mtandao wa Kibinafsi wa Virtual (VPN) kuongeza safu ya ziada ya usalama.
4. 4G au 5G inatumia data Zaidi kuliko 3G
Imani maarufu ni kwamba 4G hutumia data zaidi ya 3G. Kwa kweli, 4G au 5G ni ya kasi na muunganisho wa haraka hutumia data zaidi? Sivyo. Katika muktadha huu, "data" inahusu idadi ya habari inayotiririka kati ya mtandao na kifaa chako.
Kwa hivyo, ukipakua picha ya 2MB ukitumia unganisho la 4G, inaweza kuchukua muda kidogo kuliko kutumia 3G - lakini bado itatumia data 2MB haswa. Jambo hilo hilo litakuwa kweli wakati 5G inapotumika.
Kwa kifupi, kitu pekee ambacho ni tofauti kati ya vizazi vya teknolojia ya rununu ni kuathiri kasi ya unganisho lako.
4. Simu za rununu hutoa mionzi yenye Madhara
Tangu simu za rununu zilipoletwa sokoni mara ya kwanza, watu wamekuwa na wasiwasi kwamba mionzi inayotolewa nazo ni hatari - inasababisha saratani na magonjwa mengine mabaya.
Lakini uelewa mdogo huenda ukasaidia kuondoa hofu hiyo .
Katika kesi hii, tunachohitaji kuelewa ni nini simu za rununu hutoa.
Jibu ni mawimbi ya umeme: vitu sawa ambavyo hufanya redio yako ifanye kazi. Mionzi ya umeme ya masafa ambayo simu za rununu hutoa ni salama kabisa.
Kwa kweli, zaidi ya nakala 25,000 zimeandikwa juu ya athari ya mionzi ya umeme kwa wanadamu - ambayo ni utafiti zaidi kuliko tuliofanyia kemikali nyingi kwenye chakula chetu.
6. Usitumie simu yako yako wakati inachaji
Unaweza kupata shida kuweka simu yako chini. Kwa kweli, ni muhimu kwa maisha yako ya kijamii, wakati wako wa kupumzika, labda afya yako na hata ununuzi wako mitandaoni .
Dhana kwamba haupaswi kutumia simu yako wakati inachaji, basi, ni ile ambayo watu wengi wangependa kuona ikipuuzwa .
Na ukweli ni huo kwamba hii ni dhana tu bali haina ukweli . Kuna vifaa vingine vya elektroniki ambavyo si salama kutumia wakati wa kuchaji (ambayo labda ni jinsi dhana hii ilianza kutumika ), simu za rununu sio moja wapo.
Kwa kweli, ikiwa unatumia simu yako wakati inachaji, itachukua muda mrefu betri kujaa , Lakini haitakudhuru wewe au simu yako.
CHANZO- BBC SWAHILI