Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KILICHOJIRI MAHAKAMANI KATIKA KESI YA FREEMAN MBOWE NA WENZAKE

Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe  na wenzake watatu wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi leo  imeanza kusikilizwa mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

Leo kesi hiyo inaendelea katika hatua ya usikilizwaji wa pingamizi la awali lililowekwa na washtakiwa kupitia kwa jopo la mawakili wao 14 wakiongozwa na Peter Kibatala.

Katika pingamizi hilo washtakiwa hao wanadai kuwa hati ya mashtaka ina kasoro za kisheria pamoja na mambo mengine wakidai kuwa sheria ya ugaidi ambayo wanashtakiwa nayo haijafafanua viambato vya kosa la ugaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com