MAHAFALI YA 16 YA SHULE YA MSINGI BUHANGIJA JUMUISHI YAFANYIKA...WANAOFICHA WATOTO WENYE ULEMAVU WAPEWA UJUMBE


Wanafunzi waliohitimu elimu ya Msingi katika Shule ya Buhangija Jumuishi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali .

Na Marco Maduhu, Shinyanga

SHULE ya Msingi Buhangija Jumuishi iliyopo Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga imefanya mahafali ya 16 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi shuleni hapo, huku wazazi wakionywa kuacha tabia ya kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu, bali wawapatie haki yao ya kielimu na kutimiza ndoto zao.

Mahafali hayo yamefanyika leo Alhamisi Septemba 30,2021 kwenye ukumbi wa mikutano katika mabweni ya kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali ambao wanasoma shuleni hapo, huku mgeni Rasmi akiwa Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo.

Akizungumza kwenye Mahafali hayo Mgeni rasmi Sabo, amewataka wazazi hapa nchini kuacha kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu, bali wawapeleke shule kama watoto wengine, ili watimize ndoto zao na kuja kuwasaidia hapo baadae.

“Nimefurahishwa namna shule hii inayotoa elimu kwa watoto wote bila ya kujali wenye ulemavu, na wamekuwa wakifanya vizuri sana katika mitihani yao, hivyo natoa wito kwa wazazi wasione kuzaaa mtoto mwenye ulemavu kuwa ni mkosi, bali wawapatie haki yao ya elimu na siyo kuwaficha ndani,”alisema Sabo.

Aidha, alitoa wito kwa wazazi kuwalinda watoto wao ambao wamehitimu elimu ya msingi na kubaki majumbani, wawalinde na kuwapeleka kupata masomo ya maandalizi ya kuingia kidato cha kwanza, na siyo kupanga kuwaozesha ndoa za utotoni na kuzima ndoto zao.

Katika hatua nyingine, amewataka wanafunzi watakapoanza masomo yao ya kidato cha kwanza mwaka 2022 wakajitume pamoja na kudumisha nidhamu ya hali ya juu ili wafikie malengo yao.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Fatuma Jilala, akitoa neno kwenye mahafali hayo, amewataka wanafunzi hao wasiende kuzurura mitaani, wala kujiingiza katika makundi mabaya yakiwamo ya uchangudoa, na madawa ya kulevya bali wajitunze, na matokeo yakitoka ya kujiunga na kidato cha kwanza wakutwe wakiwa salama.

Nao wahitimu wa elimu hiyo ya msingi katika Risala yao iliyosomwa na Pactamedy Mwita, wamesema walianza elimu ya msingi mwaka 2015 wakiwa 133, na leo wamehitimu 120, wavulana wakiwa 62 wasichana 58, huku wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali wakiwa 12.

Pia katika Risala hiyo wanafunzi hao wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali, na kuwapatia wenzao wenye ulemavu mashine ya kuchapisha maandishi ya Nukta Nundu, Vifaa vya kuongeza usikivu, pamoja na miwani ya kukuza maandishi kwa wale wanafunzi wenye matatizo ya uoni hafifu.

Wameongeza kuwa, shule hiyo wamejengewa vyoo vya kisasa vyenye kuzingatia mahitaji maalumu, Madarasa, pamoja na kujengewa uzio wa kuzunguka mabweni yao na kuimarisha ulinzi zaidi.

Mgeni Rasmi diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo, akizungumza kwenye Mahafali ya darasa la Saba katika Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Fatuma Jilala akizungumza kwenye Mahafali hayo.

Mhitimu wa elimu ya msingi Pactamedy Mwita akisoma Risala katika Mahafali hayo.

Muonekano wa keki ya Mahafali ya 16 katika Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi.

Wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wageni waalikwa na wazazi wakiwa kwenye Mahafali hayo.

Wageni waalikwa na wazazi wakiwa kwenye Mahafali hayo.

Mgeni Rasmi Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo, akigawa vyeti wa wahitimu.

Zoezi la ugawaji vyeti kwa Wahitimu likiendelea.

Zoezi la ugawaji vyeti kwa Wahitimu likiendelea.

Zoezi la ugawaji vyeti kwa Wahitimu likiendelea.

Wahitimu wakitoa burudani.

Wahitimu wakiendelea kutoa burudani huku Mgeni Rasmi akitoa zawadi.

Walimu wa shule hiyo wakitoa Burudani.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post