KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Gerald Kusaya akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu iliyokuwa ikiongozwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira Patrobas Katambi wa kwanza kushoto na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt Alice Kaijage |
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt Alice Kaijage ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Gerald Kusaya kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira Patrobas Katambi |
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Clemence Marcel akitoa tarifa ya uanzishwaji wa utaoji wa huduma ya Methadone kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu |
MJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Mh Neema Lugangira (MB) akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Gerald Kusaya amesema kwa sasa mapambano ya kudhibiti dawa za kulevya hapa nchini wameyapa sura mpya kwa kujipanga kufanya doria baharini na operesheni mbalimbali ndani ya nchi.
Kusaya aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu iliyokuwa ikiongozwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira Patrobas Katambi.
Ambapo walipotembelea na kujionea maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Utoaji wa Huduma ya Methaadone (MAT CLINIC) Hospitali ya Bombo,Asasi (Gift of Hope) inayoibu waraibu kwenda kupata huduma MAT)
Pamoja na kutembelea nyumba 3 za upataji nafuu (Sober Houses) ambazo ni Courage on Recovery Foundation,Tanga Drug Free, na Gift of Hope ambapo lengo la ziara hiyo ni kuwapitisha wabunge kwenye shughuli za matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya ili waweze kujionea wenyewe jinsi shughuli hizo zinavyofanyika.
Alisema pia na wanawashukuru wananchi kwa kushirikiana kwa karibu kwenye mapambano hayo huku akieleza hayo ni mambo mtambulika na hayawezi kufanywa na Taasisi moja hivyo wanafanya kwa ujumla kama Taifa na kushirikiana na mataifa mengine kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.
“Ki ukweli sisi kama Mamlaka tumejipanga imara kuhakikisha tunadhibiti uingiazwaji wa dawa za kulevya hapa nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo nchi kavu na majini kwa sababu kumbukumbu zinaonyesha kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kilikuwa kinaingia kwa kupitia ukanda wa bahari”Alisema
Alisema kwa sababu ukanda huo ni mkubwa sana toka Tanga, Lindi hadi Mtwarani una eneo kubwa na kuna maeneo mengine ya Bandari Bubu yanayotumiwa na wahalifu kuingiza dawa za kulevya hiyo wamejipanga kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kuhakikisha haziiingiii.
Kamishna huyo alisema wao kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama watahakikisha usalama unakuwepo ndani ya bahari ili kuweza kudhibiti uingiaji wake ambapo alisema hilo wamelifanya na ndio maana hivyo sasa wameanza kuitokomeza.
Hata hivyo alisema cha pili kitakachofanyika ni kuendelea kuwapa matibabu watu ambao wameathirika na dawa za kulevya huku akitoa wito kwa jamii kubadilika na watambue kwamba lazima wawapokee, wawapende na kuwajali na kuwathamini.
Kamishna huyo aiitaka jamii kuacha kuwatenga watu wanaotumia dawa za kulevya badala yake waweze kuwa karibu na vijana hao kuhakikisha hawatumie dawa hizo.
“Lakini niseme tu kwamba mpaka sasa hapa nchini kuna vituo 11 vya kupata dawa kwa waraibu ambao kimsingi wameamua kubadilika na kuamua kuachana na utumiaji wa dawa hizo…pia niitake jamii iacha kuwanyanyapaa watumiaji ambao wameamua kutokutumia”Alisema
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira Patrobas Katambi aliannza kwa kuipongeza Mamlaka ya Kupambana na Kdhibiti dawa za Kulevya nchini Kwa hatua ya mapambano ya kudhibiti dawa za kulevya hapa nchini kwa sababu vita imepiganwa vilivyo na imeelezwa kwenye ilani ya CCM kwamba watapambana nayo.
Alisema kutokana na kwamba dawa za kulevya zimekuwa na madhara makubwa kuliko faida dunia na nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko kwa sababu ya kutumia vijana kuingia kwenye wimbi la dawa za kulevya matokeo wanapata madhara ya kiafya ambayo yanakwenda kwenye familia zao na jamii kwa jumla.
Naibu Waziri huyo alisema kwa sehemu kubwa kwa sababu ya kutumia madawa wanakuwa hawapo kwenye ufahamu wa kawaida mara nyingi wamekuwa wakitumika kwenye ugaidi,ikiwemo ngono zembe matokeo yake wanapata ukimwi na magonjwa mengine
Hata hivyo alisema kikubwa cha hatari wanakuwa hawana cha kupoteza na wanahatarisha maisha ya familia,usalama wa nchi na wengine madhara ya dawa za kulevya ni makubwa kuliko tunavyofikia kwani hupelekea kusababisha vita ya kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Social Plugin