Mkutano wa 18 wa
baraza la mawaziri wa mazingira wa nchi za Afrika –AMCEN umefanyika leo tarehe
16 Septemba 2021 ukiwa umebeba kauli mbiu ya inayosema “Kulinda ustawi wa watu na kuhakikisha utunzaji endelevu wa mazingira Afrika”.
Akizungumza kabla
ya kuanza kwa mkutano huo kwa njia ya mtandao Mkurugenzi wa Shirika la
Mazingira la Umoja wa Mataifa - UNEP
kanda ya Afrika Dokta Juliette Biao Koudenoukpo amesema mawaziri wa mazingira
kutoka nchi 54 za Afrika wanakutana kila baada ya miaka miwili au mitatu
kujadili masuala yanayohusu mazingira katika nchi zao.
Dokta Koudenoukpo amesema
mkutano wa AMCEN kwa kawaida unatanguliwa na kikao cha wataalamu wa mazingira Afrika
kilichofanyika tarehe 13 na 14 Septemba mwaka huu.
Dokta Koudenoukpo ameeleza
kuwa kwa kuwa mkutano wa wakati huu umefanyika kukiwa na tatizo la ugonjwa wa
CORONA duniani hiyo agenda zimegawanywa katika sehemu kuu mbili, ya kwanza
ikiwa ni kushughulikia masuala ya haraka ya uratibu ya AMCEN ambapo ya pili ni
kukubaliana kuahirisha yale masuala yanayohitaji mazungumzo hadi mwaka ujao wa
2022.
Mkutano huo
umewaleta pamoja wawakilishi wa nchi 54 za Afrika wanachama wa AMCEN pamoja na
wadau mbalimbali kutoka kwenye wizara za nchi wanachama, mashirika binafsi,
mashirika ya kijamii, wadau wa maendeleo na taasisi za umoja wa mataifa.
Mkutano wa mwaka huu umeongozwa na Rais wa AMCEN Waziri wa mazingira, Misitu na uvuvi wa Afrika Kusini Bi Barbara Creecy.
AMCEN imeanziashwa
mwaka 1985 kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kikanda kati ya serikali za
Afrika na washirika wao katika kushughulikia changamoto za mazingira
zinazojitokeza.
Kupitia AMCEN
serikali za nchi wanachama zimeimarisha sera za mazingira na kushirikiana na
asasi za kiraia na sekta binafsi katika kuimarisha ulinzi na uhifadhi endelevu
wa mazingira Afrika.
Social Plugin