MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ametoa wiki moja kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaofanya biashara ya ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi baada ya suala hilo kulalamikiwa na wananchi.
Malalamiko hayo yametolewa wakati wa mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.
Kutokana na hilo, RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.
Aidha, RC Makalla ameelekeza viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.
Social Plugin