Mshtakiwa wa pili Adam Kasekwa, katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amemamliza kutoa utetezi wake kwenye shauri dogo la kesi hiyo.
Kasekwa amemamliza kutoa ushahidi wake leo Jumatatu, tarehe 27 Septemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mustapha Siyani, baada ya kuulizwa na kuhojiwa na mawakili wa utetezi pamoja na mawakili wa Jamhuri.
Kasekwa alianza kutoa ushahidi wake Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021, katika kesi hiyo ndogo ndani ya kesi kubwa iliyotokana na pingamizi la utetezi kupinga maelezo yake ya onyo yasitumike mahakamani hapo kama ushahidi, kwa madai yalichukuliwa kinyume cha sheria.
Tangu alipoanza kutoa ushahidi wake mahakamani hapo, Kasekwa amedai mchakato uliotumika kumkamata, kumuweka kizuizini na uandikishwaji wa maelezo yake ya onyo hayakufuata sheria.
Social Plugin