Ajali iliyopelekea kifo cha Mwandishi wa ITV na Radio One, Gabriel Kandonga
Mwandishi wa Habari wa ITV na Radio One mkoani Songwe Gabriel Kandonga, amefariki dunia kwa ajali ya gari.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Septemba 24, 2021, wakati akitokea nyumbani kwake Mpemba kuelekea wilayani Songwe katika majukumu yake ya kila siku.
Inaelezwa kuwa alikuwa njiani kuungana na kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na Dawa za Kulevya ambayo inaendelea na ziara yake wilayani Songwe
Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba, amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwandishi huyo na kusema ajali hiyo imetokea katika eneo la shule ya Sekondari Mlowo ambapo alikuwa anajaribu kulipita lori na hatimaye kulivaa fuso kwa upande wa nyuma.
Social Plugin