NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetekeleza ahadi waliyoiahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 26 kwaajili ya kukarabatti mabweni ya shule ya Sekondari Jitegemee iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule amesema msaada walioutoa utawasaidia wanafunzi kupata mazingira mazuri ya kulala hivyo amewasihi wanafunzi kutunza miundombinu ya shule hiyo ili kuweza kuipendezesha shule hiyo.
Aidha Bw.Mwakifulefule amesema Shirika hilo litatuma wataalamu kwaajili ya kutoa elimu kuhusu bima ili waweze kuelewa umuhimu wa kuwa na Bima ya NIC paamoja na kuwa mabalozi wazuri pindi wakiwa katika jamii.
"Nimemuahakikishia Mkuu wa shule wiki ijayo nitatuma vijana watakuja hapa kuwapeni shule ya bima ili muweze kuelewa namna ya kutumia huduma za bima zenye bei rahisi lakini manufaa yake ni makubwa zaidi tena vijana hao walisoma hapahapa Jitegemee". Amesema Bw.Mwakifulefule.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee Kanali Robert Kessy ameushukuru uongozi wa NIC kwa kuweza kutekeleza ahadi waliyoiahidi kutoa fedha kwaajili ya kukarabati mabweni katika shule hiyo.
"Niwapongeze NIC kwa kuja kutukabidhi rasmi ile thamani ambayo waliahidi ya Milioni 26 tumeona mfano wa vitu ambavyo vitatumika kwenye huo ukarabati". Amesema Kanali Kessy.
Aidha amesema uamuzi huo wa kuwasaidia ulitokana na ombi lao walilowasilisha kwenye mahafali ya kidato cha sita mwaka huu ambapo waliwasilisha kutokana na hitajio baada ya kufanyika kwa ukaguzi.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameushukuru uongozi wa NIC na kuahidi kuendelea kulinda na kuthamini mchango ambao umetolewa na shirika hilo na kuwafanya kuishi katika mazingira mazuri ya masomo.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule (kulia) akikabidhi baadhi ya mabati kwa Mkuu wa Shule ya Sekondati Jitegemee Kanali Robert Kessy kwaajili ya ukarabati wa mabweni ya shule hiyo.Hafla hiyo imefanyika leo katika shule hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule (kulia) akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkuu wa Shule ya Sekondati Jitegemee Kanali Robert Kessy kwaajili ya ukarabati wa mabweni ya shule hiyo.Hafla hiyo imefanyika leo katika shule hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule akizungumza mara baaa ya kukabidhi msaada wa Shilingi Milioni 26 za ukarabati wa mabweni ya shule ya Sekondari Jitegemee leo Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Shule ya Sekondati Jitegemee Kanali Robert Kessy akizungumza mara baada ya Shirika Bima la Taifa (NIC) kutoa msaada wa Shilingi Milioni 26 kwaajili ya kukarabati mabweni ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Sekondari Jitegemee Brigedia Jenerali (Mstaafu) Lawrence Magere akizungumza mara baada ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoa msaada wa Shilingi Milioni 26 kwaajili ya kukarabati mabweni ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Jitegemee kidato cha Sita Faidh Robert akitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) mara baada ya kupokea zawadi ya shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati mabweni ya shule hiyo.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Jitegemee kidato cha Sita Hamza Abeid akitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) mara baada ya kupokea zawadi ya shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati mabweni ya shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Jitegemmee wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya Shirika Bima la Taifa (NIC) kutoa msaada wa Shilingi Milioni 26 kwaajili ya kukarabati mabweni ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule akipata picha ya pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee mara baada ya kufika na kutoa msaada wa Shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati wa Mabweni ya shule zao.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule akipata picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na walimu wa Shule ya Sekondari Jitegemee mara baada ya kufika na kutoa msaada wa Shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati wa Mabweni ya shule zao.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Social Plugin