Meneja uhusiano wa Shirika la Bima la Taifa NIC, Bw.Karimu Meshack akikabidhi mfuko wa unga wa ngano kwa mwanzilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Lady Fatima Bw.Kalekela Omary mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula katika kituo hicho.
Watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakipata picha ya pamoja na watoto yatima mara baada ya kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Kigamboni Jijini dar es Salaam.
Meneja Uhusiano kutoka NIC Karimu Meshack akipata picha ya pamoja na watoto yatima mara baada ya kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Lady fatima kilichopo Kigamboni Jijini dar es Salaam.
**************************
SHIRIKA La Bima la Taifa (NIC,) limetembelea na kutoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulea watoto yatima cha Lady Fatima kilichopo Kigamboni ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera kurudisha kwa jamii inayoyekekezwa na shirika hilo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Meneja Uhusiano kutoka NIC Karimu Meshack amesema sera ya shirika hilo ni kurudisha kwa jamii pamoja na miradi ya Serikali inayogusa jamii moja kwa moja hasa watoto, wanawake na wazee.
Karimu amesema, baada ya kuona uhitaji wa chakula katika kituo hicho wakaona ni vyema kuungana na kituo hicho kinacholea watoto yatima wapatao 25.
"NIC daima tupo karibu na jamii, na leo tumekuja kuwatembelea watoto wetu na kuwaletea mahitaji yatakayosaidia katika ukuaji wa watoto wetu ikiwemo unga wa sembe na ngano, mchele, maharage na mafuta ya kupikia." Amesema.
Aidha amesema, Shirika hilo lipo pamoja na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma za msingi ikiwemo afya na elimu zinawafikia wananchi.
Kwa upande wake mwanzilishi wa kituo cha Lady Fatima Bw. Kalekela Omary ameishukuru NIC kwa kuwatembelea na kutoa msaada wa chakula kwa watoto hao na kuwakaribisha wadau wengine kufuata nyayo za NIC katika kushiriki kuwalea watoto hao kwa namna mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.
Social Plugin