Jeshi la Polisi limewafukiza kazi askari wake 7 wa kituo cha Polisi Wilaya ya Ileje baada ya kukutwa na kosa la kuvuka mpaka wa Tanzania na kuingia Malawi wakiwa wamevaa sare za Jeshi na silaha za moto kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Janneth Magomi amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya askari hao kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi Septemba 20, 2021 na kuwakuta na hatia.
Via Mwananchi
Social Plugin