RAIS SAMIA ATUMBUA MAWAZIRI....KIJAJI AMRITHI FAUSTINE NDUGULILE, JANUARY MAKAMBA AKAA NAFASI YA KALEMANI, DKT. TAX AJAZA YA KWANDIKWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 12, 2021 amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi kama ifuatavyo:-

  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Dkt. Kijaji anachukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile (Mb), ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha, Rais ameihamishia Idara ya Habari katika Waziri ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Wizara mpya itafahamika kama Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Stergomena Tax (Mb), kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Dkt. Tax anachukua nafasi ya Marehemu Elias John Kwandikwa.
  2. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua January Makamba (Mb), kuwa Waziri wa Nishati. Makamba anachukua nafasi ya Dkt. Merdard Kalemani (Mb), ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Makame Mbarawa (Mb), kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Prof. Mbarawa anachukua nafasi ya Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (Mb), ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Eliezer Feleshi, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Feleshi alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post