Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Septemba 18, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia baraza hilo.
Pamoja na Mkutano huo, Rais Samia pia atahudhuria mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
Aidha, anatarajiwa pia kukutana na wakuu wa nchi nyingine na viongozi wa mashirika ya kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.
Social Plugin