Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC SINGIDA AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA BOMBA LA MAFUTA

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza jana wakati akifungua mkutano wa wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida kuhusu fursa zitakazopatikana wakati wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Kushoto ni KatibuTawala Mkoa wa Singida  Dorothy Mwaluko na Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Safiel Msovu.
KatibuTawala Mkoa wa Singida  Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Safiel Msovu akizungumzia mradi huo.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Waandishi Wetu, Singida

MKUU  wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka wananchi mkoani hapa kutumia fursa zitakazopatikana wakati wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) utakaoanza hivi karibuni ili waweze kujiongezea kipato na kuondoa umaskini.

Dkt.Mahenge ametoa wito huo jana wakati akifungua mkutano wa wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida na kuwataka kuzitumia fursa mabambali ambazo zitapatikana wakati wa ujenzi wa bomba hilo.

Alisema ujenzi wa bomba hilo utakuwa na jumla ya vituo 14 katikaWilaya na  Mikoa mbalimbali ambapo kituo cha  11 kitakuwa mkoani Singida katika Kijiji cha Ntondo kilichopo Manispaa ya Singida Mjini.

Dkt. Mahenge alisema kituo hicho kitakuwa na watumishi kuanzia 1,000 hadi 2,000 ambao watahitaji kula,kulala na kunywa hivyo wananchi wa Singida wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuanza kuwekeza kwa kujenga vyumba za kupangisha, nyumba za kulala wageni pamoja na ufugajiwa kuku ili wapate kipato na watoe ajira kwa wengine.

Aidha Serikali tayari imeandaa mazingira wezeshi yanayovutia uwekezaji kwa kutengeneza barabara na kuweka umeme ili wananchi wawezekuendelea na mapambano ya kuondoa umasikini alifafanua Mahenge.

 Mahenge alisema kwamba Serikali mkoani hapa imeendelea kuzungumza na mabenki mabalimbali wapunguze riba katika mikopo yao ili iwezekuwavutia wateja.

KatibuTawala Mkoa wa Singida  Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa ni mmoja wa wadau katika mkutano huo alisema bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 140  kwa Singida ambapo litapita katika wilaya tatu za Iramba, Mkalama na SingidaVijijini.

Alisema jumla ya vijiji 31 na kata 17 vitapitiwa na mradi huo hivyo aliwataka wananchi wa maeneo husika kuhakisha wanatumia fursa kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Safiel Msovu akizungumzia mradi huo alisema kwamba bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,448 ambapo litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 216 kwa siku.

Alisema mradi huo ni mkubwa na unagharimu kiasi cha dolabilioni 3.5 sawa na sh.Trilioni nane (8)na  unatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kuwa mikataba muhimu imekamilika.

“Wanahisa katika mradi huo ni Kampuni ya Ufaransa inayojulikana kwa jina la Total, Uganda kupitia Shirika la Mafuta la  UNOC , Kampuni ya Kichina ya CNOOC na Shirika la Uendelezaji wa Petrol nchini (TPDC)” alisema Msovu.

Kwa mujibuwa  muundo wa sasa wa mgawanyo wa hisa, Kampuni yaUfaransa Total itamiliki asilimia 62, kampuniya China CNOOC asilimia 8, UNOC ya Uganda itamiliki asilimia 15 na asilimia15 iliyobaki itamilikuwa na Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Msovu alisema mradi huo unategemewa kujengwa kwa kipindi cha miaka mine (4) na unategemewa  kutoahuduma kwa miaka isiyopungua 25.

Wafanyabiashara mkoani hapa kwa umoja wao wamesema wamejipanga kutumia fursa hiyo na wameiomba Serikali kuendelea kutengeneza mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusiana na maendeleo ya mradi huo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com