Na Magrethy Katengu_Dar es salaam
Ikiwa imesalia siku moja kuelekea siku ya maadhimisho ya kupata taarifa, Umoja wa asasi zinazotetea haki ya kupata taarifa (CoRI) umeziomba taasisi zote za kiserikali na zisizo za kiserikali kuzingatia kifungu cha sheria yakikatiba ubara ya 18 ya haki ya kupata taarifa kama ilivyotungwa na bunge miaka iliyopita.
wito huo umetolewa leo na CORI, ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya kimaifa ya siku ya haki ya kupata taarifa ambayo ni Septemba 28 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kitaifa itaadhimishwa Dar es salaam katika ukumbi wa kimataifa Mwalimu Kambarage Nyerere
Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Umoja wa asasi zinazotetea haki ya kupata taarifa (CoRI) Kajubi Mukajanga wakati akitoa tamko la pamoja kuelekea siku hiyo amesema ni nusu muongo sasa tangu kupitishwa na bunge sheria ya haki kupata taarifa lakini utekelezaji wake ni hafifu kumekuwa matukio ya Waandishi wa habari wawapo katika majukumu yao mtoa habari kuhitaji aandikwe anavyotaka yeye.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Tahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema kila mtu anayo haki ya kutafuta,kupatiwa na kusambaza taarifa,katiba pia ina tamko la kimataifa la haki za binadamu kama sehemu ya maudhui yake likitamka uhuru wa maoni,kujieleza na kujumuika
"Tunataka kuteuliwa kwa maofisa watoa taarifa katika kila taasisi ya Umma wenye mamlaka na wajibu wa utoaji taarifa za mara kwa mara na zile zinazoombwa na mwananchi mmoja mmoja kama inavyotamkwa na kifungu cha 7cha sheria",alisema Balile.
Hata hivyo amesema kuna umuhimu wa kuanzishwa mfumo wa ufuatiliaji kubaini maombi yote ya taarifa na majibu yake katika taasisi za Umma ili kuepusha malalamiko baadhi ya waandishi kuwa barua za maombi wanapohitaji taarifa kutojibiwa au kukaa muda mrefu bila majibu
Meneja utetezi kutoka twaweza Anna Rugamba amesema CoRI inaamini kuwa ipo haja ya marekebisho ya sheria ya huduma za vyombo vya habari ys mwaka 2016,kuongeza kasi ya Utekelezaji wa sheri haki ya kupata taarifa pamoja na maboresho na utekelezaji wa kanuni za sheria hizo.