Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC WAACHIA JEZI MPYA


Muonekano wa jezi mpya za klabu ya Simba zitakazotumika mechi za nyumbani msimu wa 2021/22 kwenye mashindano mbalimbali.

KUELEKEA kilele cha siku ya Simba (SIMBA DAY) Septemba 19, mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, klabu hiyo imeachia rasmi jezi zitakazotumika msimu ujao ambazo tayari zimeanza kuuzwa licha ya hapo awali kutangaza kuwa uzinduzi rasmi ungefanyika Septemba 4 (kesho).

Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga kuanza kuuzwa kwa jezi hizo ni kutokana na mahitaji makubwa ya mashabiki wao, hivyo wameheshimu hilo na kuziweka hadharani.
Jezi za ugenini
Jezi chaguo la tatu


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com