TANESCO WATOA ELIMU KATIKA VIJIJI VINAVYOFADHILIWA NA REA


Afisa uhusiano huduma kwa wateja Mkoa wa Simiyu Bw.Ben Kirumba akitoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Masewa wilayani Bariadi kuhusu Mradi wa REA III Mzunguko wa II


Afisa uhusiano huduma kwa wateja Mkoa wa Simiyu Bw.Ben Kirumba,akitoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Masewa wilayani Bariadi kuhusu matumizi ya kifaa cha UMETA - umeme tayari kama mbadala wa kufanya wiring katika nyumba ndogo kinachopatikana kwa gharama ya sh 36,000


Afisa uhusiano huduma kwa wateja Mkoa wa Simiyu Bw.Ben Kirumba,akitoa elimu kwa wananchi wa Kijiji cha Matongo kuhusiana na matumizi ya umeme.


Afisa Masoko kutoka Makao Makuu Dodoma Adelina Iyakurwa,akitoa elimu kwa wananchi wa Kijiji cha Kidabu wilayani Maswa kuhusiana na matumizi ya umeme pamoja na kifaa cha UMETA - umeme tayari kama mbadala wa kufanya wiring katika nyumba ndogo kinachopatikana kwa gharama ya sh 36,000


Afisa Masoko kutoka Makao Makuu Dodoma Adelina Iyakurwa,akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme na usalama wa umeme kwa wanafunzi wa shule za Msingi wilayani Itilima Mkoani Simiyu

.............................................................................

Na Mwandishi wetu,Simiyu

Jumla ya vijiji vitakavyopata umeme kupitia wakala wa umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili katika mkoa wa simiyu vipo vijiji 201 ( Bariadi 52, Maswa 29, Itilima 57, Meatu 57 na Busega 06) na muda wa mradi ni miezi 18 kuanzia julai 2021

TANESCO Simiyu kwa kushirikiana na kitengo cha Masoko kutoka makao makuu wmeanza kutoa elimu katika vijiji vinavyonufaika na mradi huu.

Wakitoa Elimu kwa wananchi wamesema kuwa wanufaika wa mradi huo ni wananchi walio mbali na miundombinu ya umeme pamoja na wananchi wote walio karibu na nguzo ndogo za kusambazia umeme ndani ya Mita 30.

''Tunawaomba wananchi wote muwe na subiri kwani huduma ya umeme mtakapata bila shida yoyote pindi awamu zijazo mara baada ya kukamilika kwa Mradi huo''

Pia wananchi wamepewa elimu kuhusiana na uwekaji mtandao wa waya katika nyumba kwa kutumia wakandarasi wanaotambulika na Serikali kupitia EWURA na TANESCO ili kuwawekea mtandao wa waya ulio bora.

Lazima mtumie wakandarasi wanotambulika ili kuepuka matapeli na Ofisi ya Mkoa TANESCO itahakikisha inapeleka orodha hiyo kwenye ofisi ya kila kijiji ili wananchi waweze kupata mafundi sahihi.

Hata hivyo wananchi wametakiwa kutumia Kifaa cha Umeme tayari (UMETA) katika vyumba visivyozidi viwili kama mbadala wa “wiring” na kifaa hiki kinapatikana TANESCO kwa shilingi 36,000 tu.

Wakizungumzi a kuhusu Utaratibu wa kupata fomu ya Maombi ya awali ya umeme Ofisi ya Mkoa itapanga utaratibu wa kupeleka fomu za maombi ya awali ya umeme katika kijiji husika kutokana na vijiji vingi kuwa mbali na Ofisi za Shirika hilo.

Pia wameelimishwa vitu pia vya muhimu wanavyotakiwa kuwa navyo ikiwa pamoja na Picha,kitambulisho ili kupata fomu ya maombi ya umeme ambayo hutolewa bure.

Amesema kuwa bei ya kuunganishiwa Umeme Kwa mwananchi anaehitaji njia moja ya umeme (Single phase) ni 27,000 na mteja anayehitaji njia tatu ya umeme (three phase) ni 139,120.74 na malipo hufanyika kupitia namba ya malipo (control number) katika mitandao ya Simu na kwa njia ya benki kupitia mfumo wa GePG pamoja njia za kununua umeme wananchi.

Kuhusu (Matumizi bora ya Umeme wananchi wameshauriwa kununu vifaa bora vya umeme ili kuweza kutumia umeme kwa usahihi pamoja na kukagua mifumo yao ya umeme kila baada ya miaka mitano .

Pia kuhusu Elimu ya Usalama Wateja wameelimishwa kutofanya shughuli za Kilimo, biashara karibu na miundombinu ya umeme na kutoa taarifa endapo wataona waya uliokatika, nguzo iliyoanguka au mlipuko katika njia kuu za kusafirishia umeme na kutochoma moto na kutokukata miti iliyokaribu na miundombinu ya umeme.

Aidha wananchi wametakiwa k Kujihadhari na Matapeli/Vishoka kwa kutotoa kiasi chochote cha pesa kwa mtu yeyote ili kuletewa nguzo au kulipia fomu ya maombi ya umeme malipo yote yanafanyika kupitia mfumo rasmi wa malipo ya serikali.

Hata hivyo wameeleza kuwa wameanza kwa kushirikiana na ofisi za wilaya kwanza ili kuutambulisha mradi huu wa REA III mzunguko wa II pamoja na kuwatambua wawekezaji wa maeneo hayo ili waweze kutambulishwa TANESCO.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post