Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, mama Rose Mrema amefariki dunia.
Taarifa kutoka kwa mume wa marehemu Mzee Augustine Mrema zimeeleza kuwa amefariki dunia Alhamisi Septemba 16, 2021 majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
“Nasikitika kutangaza kifo cha mke wangu (ROSE MREMA) kilichotokea jana tarehe 16/9/2021 saa 8 mchana Muhimbili kwa tatizo la shinikizo la damu,” Augustino Lyatonga Mrema.
Social Plugin