Muonekano wa gari baada ya ajali
Nicolaus Ngaiza enzi za uhai wake
Mwandishi wa habari wa Azam Media mkoa wa Kagera Nicolaus Ngaiza amefariki dunia usiku huu Septemba 5,2021 baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka wilaya ya Biharamulo walipokwenda kikazi kupata ajali katika eneo la Gwanseli wilayani Muleba.
Katika ajali hiyo pia mwandishi wa habari wa Clouds Media Group Benson Eustace, alikuwemo na amejeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera wodi namba nne akiendelea kupatiwa matibabu.
Ajali hiyo imetokea wakati wakiwa njiani kurudi Bukoba.
R.I.P Nicolaus Ngaiza
Social Plugin