Aliyekuwa muigizaji maarufu katika kipindi cha Gumbaru school kilichokuwa kipeperushwa kwenye runinga ya K24 Mathiokore, ameaga dunia.
Kifo chake kimetangazwa na produsa na mkurugenzi wake Kimathi Iceberg ambaye alisema sekta ya uigizaji imepata pigo kubwa.
Mathiokore alipata umaarufu baada ya kuigiza katika vipindi kadhaa ikiwemo mashtaka na vingine vya lugha ya kikuyu.
Kifo cha Mathiokore ambaye aliigiza katika vipindi vya Mashtaka, Ngumbaru na vinginevyo kilitangazwa na produza wake Kimathi Iceberg ambaye alisema sekta ya uigizaji na sanaa kwa jumla itamkosa sana akishikilia kwamba imepata pigo kubwa zaidi.
Kimathi alisema alifanya kazi na mzee hadi dakika ya mwisho lakini hivi maajuzi wakiwa naye mjini Meru, alionekana mdhaifu sana.
" Miezi minne iliyopita, tulienda Meru kushoot video flani na tuliporudi, mzee alionekana mnyonge na mdhaifu sana ila hakuwa mgonjwa, nimesikia tu kifo chake asubuhi ya leo," Alisema Kimathi.
" Alikuwa mzee mzuri sana, nakumbuka shoo yake aliyofanya ya kwanza ilivutia sana, alikuwa mtu mwenye bidii, tulifanya pamoja miradi mingi, alikuwa na talanta ila tu aliingia katika sekta ya uigizaji kama umri wake umesonga, hata hivyo tunashukuru muda tuliyokuwa naye," alisema Kimathi.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin