Mkurugenzi wa Uhusiano, Mawasiliano na Sheria wa TBL , Mesiya Mwangoka, akiongea wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Kamanda wa kikosi cha Usalam barabarani, SACP Wilbrod Mutafungwa,akiongea wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani. Kulia ni Afisa Mnadhimu wa kikosi cha Usalama Barabarani ACP Mkadam Mkadam
Maofisa wa polisi wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Maofisa wa Jeshi la Polisi na TBL katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
***
Kampuni ya TBL Plc imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, ulemavu na hasara mbalimbali.
Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wakiongozwa na Kamanda wa kikosi hicho, SACP Wilbrod Mutafungwa,uliofanyika jijini Dar es Salaam.
TBL Plc ni moja ya wadau wa kampeni za usalama barabarani nchini ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani kuendesha kampeni kwa madereva na watumiaji wa barabara kuzingatia sheria ili kupunguza matukio ya ajali nchini.
Social Plugin