Mmoja wa wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam, Abdalah Mwinyimkuu akipata chanjo kutoka kwa mtaalamu wa afya
Mke wa mmoja wa wafanyakazi wa TBL akipatiwa chanjo wakati wa zoezi hilo
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL , Jose Moran, akiongea na Mratibu wa afya wa mkoa wa Dar es Salaam, Sister Mathew (Kulia) wakati wa uzinduzi wa zoezi la Chanjo ya Covid 19 kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo . Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu Rabina Masanja, Mkurugenzi wa mawasiliano na Uhusiano Mesiya Mwangoka wa pili kulia ni mratibu wa Chanjo mkoa wa Dar es Salaam Juma Haule.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL , Jose Moran, akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la chanjo kwa wafanyakazi.
**
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19 ambapo leo imezindua zoezi la kuwapatia chanjo wafanyakazi wake katika kiwanda cha Dar es Salaam na viwanda vyake vilivyopo katika mikoa mbalimbali nchini.
Chanjo ya Covid_19 iko wazi na hiari kwa wafanyakazi wote, familia zao, na wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na jamii na kiwanda. TBL imeajiri jumla ya wafanyakazi 1,300 katika viwanda vyake 5 vilivyopo katika mikoa mbalimbali.
Uzinduzi wa Dar es Salaam umeongozwa na katibu wa Afya wa Mkoa Sister Mathew, aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk.Rashid Mfaume na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Jose Moran na Mkurugenzi wa Raslimali Watu, Rabina Masanja na wafanyakazi wa kampuni.
Moran alisema, "Chanjo kwa ujumla ni njia salama na bora ya kuzuia magonjwa na kuokoa maisha. Chanjo pia hupunguza kuenea kwa maambukizi,hiyo inamaanisha kwamba wakati tunapopata chanjo, hatujilindi tu, bali tunalinda pia wale wanaotuzunguka. Chanjo ni nafasi yetu nzuri ya kujilinda sisi wenyewe, familia zetu na wenzetu kutokana na hatari za COVID-19, na tunaamini kuwa watu wengi iwezekanavyo watatumia fursa hii kwani tutakuwa tunatoa huduma hii kwa jamii zetu ”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Rabina Masanja, alisisitiza kwamba "Afya na usalama wa wafanyakazi wetu ndio kipaumbele chetu cha kwanza. Ndio sababu tumeshirikiana na Wizara ya Afya kuhakikisha kuwa wafanyakazi wetu wote na familia zao wamepewa chanjo kwenye maeneo yetu yote ya kazi. Hii sio tu itasaidia kukuza usalama kwa kila mtu lakini pia itahakikisha mwendelezo wa biashara zetu. "
Zoezi hili la chanjo la TBL litaendelea hadi Ijumaa, Oktoba 1 katika viwanda vyote vya TBL vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.
Social Plugin