TCB YAZINDUA JUKWAA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI


Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw .Anthony Mtaka akizindua Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka akitaza bidhaa zilizotengenezwa na wajasiriamali wanawake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa sheri TCB Bi.Mystica Mapunda Ngongi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi akiwa pamoja na Mkurugenzi wa sheri TCB Bi.Mystica Mapunda Ngongi wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.Uzinduzi huo uliandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka akiwa pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi wakipata picha ya pamoja na wateja mbalimbali waliweza kufika katika uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.Uzinduzi huo uliandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka akiwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi wakipata picha ya pamojaa na Wafanyakazi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) tawi la Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.Uzinduzi huo uliandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB)
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka akiwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi wakipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.Uzinduzi huo uliandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB)

*******************************

Na Mwandishi Wetu

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imejipanga kuwa taasisi kinara ya kuwahudumia wanawake nchini hili kuwakwamua kiuchumi kupitia suluhisho za kifedha ambazo zinazingatia changamoto zao kama wajasiriamali.

Katika kutimiza hazma hiyo, TCB jana ilizindua Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo lilijikita zaidi kujadili nafasi ya akina mama katika kukuza uchumi wa taifa. Na hili kuwa na matokea chanya, Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi, alisema midahalo kama hiyo itafanyika pia Zanzibar, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.

“Katika makongamano hayo, wanawake hasa wajasiriamali, watapata fursa ya kuifahamu vizuri TCB na huduma zake wezeshi huku wakibadirishana mawazo na uzoefu wa mambo mbalimbali,” Bw Moshingi aliwaambia washiriki.

Aidha, aliongeza kuwa jukwaa hilo litazingatia sana nafasi ya wanawake kuwa chachu ya uchumi na maendeleo na jinsi wanavyoweza kutumia fursa za kibiashara zinazopatikana TCB kupitia huduma na suluhisho zake mbalimbali.

Bw Moshingi alisema benki hiyo ina wajibika kuupa kipaumbele uwezeshaji wa wanawake baada ya serikali kuziunganisha shughuli zake na zile za iliyokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB).

“Uongozi wa Benki ya Biashara Tanzania unapenda kuishukuru Serikali kwa kuwa na imani na sisi na kuamua kutuunganisha na benki za TWB, Twiga Bancorp na TIB Corporate,” Bw Moshingi alisema katika wasilisho lake.

Hatua hiyo imeiimarisha TCB sokoni kiushindani na kuifanya iwe na msuli wa kifedha wa kuweza kulihudumia taifa kwa ufanisi.Hilo aliliweka bayana kupitia takwimu za kiutendaji zinazoonyesha mali na amana za TCB kuwa 1.04trn/- na 888bn/- mtawalia kufikia mwishoni mwa mwaka jana.

Wakati faida kabla ya kodi ya TCB iliongezeka kutoka 400m/- mwaka 2007 hadi 21bn/- mwaka 2020, ukopeshaji ndani ya kipindi hicho ulikua hadi 618bn/- kutoka 36bn/-.

Bw Moshingi pia alisema zipo huduma maalum zinazowalenga akina mama kama akaunti ya TABASAMU, dirisha maalum kwa ajili yao kwenye matawi yote ya benki na huduma za bima maisha kwa vikundi ambavyo wanachama wake wengi ni wanawake.

“Mikopo zaidi 120bn/- imetolewa kwa wanawake na tumekusanya amana za 11.9bn/- kupitia akaunti za vikundi zaidi ya laki tatu ambapo asilimia 85 ya wanachama wake ni wanawake,” mtendaji huyo alisema.

Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la ufunguzi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka, ambaye aliipongeza Benki ya TCB na viongozi wake kwa kuanzisha utaratibu huo wa kimaendeleo na kiuwezeshaji.

Alisema ubunifu huo wa hali ya juu ni nyenzo mahsusi ya kuwakomboa wanawake kifedha na kuwajengea uwezo kibiashara huku akiitaka benki hiyo kuwaonyesha fursa ilizonazo za kuwasaidia.

Kwa mujibu wa maofisa waandamizi wa TCB, lengo la jukwaa hilo si tu kuwawezesha wanawake wa Kitanzania kiuchumi bali pia kuwaimarisha kifedha na kuwajenga kibiashara ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

Walisema Jukwaa la Wanawake na Biashara la TCB linaendana na mpango wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika kusimamia na kumiliki uchumi wa taifa.

“Kwa muktadha huo benki na taasisi nyingine za fedha nchini zinawajibu wa kushiriki kutekeleza ajenda hiyo ya serikali na TCB imeonyesha mfano mzuri wa hilo,” walifafanua.

Jukwaa hilo jipya litaendeleza huduma jumuishi kwa ajili ya wanawake kupitia mikakati mbalimbali itakayowawezesha kufungua uwezo wao wa ujasiriamali na kuchangia mabadiliko kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa.

Pia litajikita zaidi kwenye ufumbuzi wa changamoto zinazozikabili biashara zinazomilikiwa na kuongozwa na akina mama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post