Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) upande wa taaluma Prof. Samweli Kabote akifunga maadhimisho na maonesho ya wiki ya tiba asili ya mwafrika Kanda ya Mashariki yaliyofanyika kwenye viwanja vya Soko Kuu la Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro.Mkurugenzi wa Shahada za juu utafiti, ushauri na uhawilishaji wa teknolojia Profesa. Hesron Karimuribo akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
|
Rasi wa ndani ya Sayansi Asili na Tumizi Profesa Karugila akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufunga maonesho hayo.Mhitimu wa shahada ya kemia ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Peter Kapinga (kushoto) akimuelekeza jambo mgeni rasmi kabla ya kumkabidhi zawadi kama shukrani na kuonesha kuwa elimu waliyoipata imekuwa na mafanikio kwao kwa kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe na kufikia kushiriki maonesho hayo ya tiba asili.
Mgeni rasmi akipita kukagua na kujionea bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kuoneshwa kwenye maonesho hayo ya Tiba Asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki.Mgeni rasmi akipita kukagua na kujionea bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kuoneshwa kwenye maonesho hayo ya Tiba Asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki.
Mgeni rasmi akipita kukagua na kujionea bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kuoneshwa kwenye maonesho hayo ya Tiba Asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki.
Mgeni rasmi akipita kukagua na kujionea bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kuoneshwa kwenye maonesho hayo ya Tiba Asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki.
Mgeni rasmi akipita kukagua na kujionea bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kuoneshwa kwenye maonesho hayo ya Tiba Asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki.
Mgeni rasmi akipita kukagua na kujionea bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kuoneshwa kwenye maonesho hayo ya Tiba Asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki.
Na Calvin Gwabara, Morogoro
WAGANGA wa
tiba Asili na Tiba Mbadala wana mchango mkubwa katika jitihada za Serikali na
Wananchi katika kuendeleo kwa kaya na Taifa kwa kuhakikisha wanatoa tiba na
kuboresha afya za watanzania na hivyo kuwezeesha jamii kushiriki kwenye
shughuli za maendeleo.
Kauli hiyo
imetolewa na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) upande wa Taalama Profesa. Samweli Kabote wakati akifunga maadhimisho na maonesho
ya wiki ya tiba asili ya mwafrika Kanda ya Mashariki yaliyofanyika kwenye
viwanja vya Soko Kuu la Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro yaliyowakutanisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamni ya mimea dawa kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania.
’’Takwimu
zinaonyesha kuwa tiba asili inachngia kwa kiasi cha silimia 45% katika kutoa
huduma za afya kwa Watanzania na asilimia 55% ndio madawa mengine ya madukani
kwahiyo asilimia hizo sio ndogo kama ambavyo watu wengi wanadhani maana naamini
wengi zaidi wanaikimbilia tiba asili katika kutatua changamoto zao mbalimbali
za kiafya na hivyo kupata afya ya kuwawezesha kufanya kazi za
kiuchumi’´alisistiza Profesa. Kabote.
Aidha
amewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala sasa kuendelea na juhudi za
kuboresha dawa hizo kwa kushirikiana na watafiti wa SUA na Chuo cha Afya
Muhimbili na taasisi zingine za kupima ubora na usajili ili zizidi kuaminika na
jamii nzima bila kujali elimu ya mtu,kipato wala rangi yake na hivyo kuongeza
soko na huduma zaidi kwa jamii na kujiongezea kipato.
Profesa.
Kabote ametoa wito kwa waganga wa tiba asili kushirikiana na watafiti kote
nchini katika kubaini miti dawa ambayo wanaona ina faida kubwa katika tiba ili
ifanyiwe utafiti zaidi na kuongeza thamani ya mimea hiyo ili kupta dawa za
kitanzania nzuri na zenye ubora wa hali ya juu kwa matumizi ya hapa nchini na nje ya nchi.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga maadhimisho hayo Mkurugenzi wa
Shahada za juu utafiti, ushauri na uhawilishaji wa teknolojia Profesa. Hesron
Karimuribo alisema Wizara ya Afya inatambua mchango mkubwa wa SUA katika
jitihada za kusaidia tiba asili nchini na ndio maana wakapewa nafasi ya kuwa
mwenyeji wa m,aadhimisho hayo kwa kanda ya mashariki.
’’ Kama mkurugenzi mwenye dhamana ya utafiti SUA tumekuwa tukihakikisha tunafanya
tafiti mbalimbali kupitia wataalamu na watfiti wa chuo chetu katika sekta ya
tiba asili kwa kushirikiana na wadau hawa ili kuboresha na kuongeza thamani
dawa zao na namna wanavyotoa huduma lakini pia kuhamasisha upandaji wa mimea
dawa ili isiweze kutoweka kwakuwa inatumiwa sana na kuvunwa kwa wingi’’ alisema
Profesa. Karimuribo.`
Ameongeza
kuwa SUA imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tafiti za
kupata dawa za kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO -19 ambapo umepata dawa
mbalimbali ikiwemo dawa maarufu ya SYNADOL ambayo iantumiwa na watanzania wengi
kwa sasa ndani nan je ya Mkoa wa Morogoro kutokana na ufanisi wake katika
kusaidia wagonjwa hao.
Akieleza
ushirikiano wa SUA na wadau wa tiba asili
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa GRILL Dkt. Faith Mabiki alisema kuwa
uaizishwaji wa jukwaa la ubunifu la wadau wa bidhaa za tiba asili nchini GRILL
ni moja kati ya mikakati mikubwa iliyozaa mafanikio makubwa katika
kuwakutanisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamani lakini pia kuwapa sauti ya
pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu nchini.
’’Sisi kama
watafiti wa SUA ambao tumekuwa tukifanya kazi karibu sana na wadau hawa wa tiba
asili tunajivunia mabadiliko makubwa tunayoyaona sasa tunapofika kwa kila
mganga wa tiba asili kwa kuona namna wanavyofungasha bidhaa zao na kutengenza
dawa katika ubora wa hali ya juu tofauti na zamani mabpo walikuwa wakiwapatia
wateja au wagonjwa wao magome ya miti,majani na kuweka kwenye mifuko isiyofaa
kuweka dawa’’alifafanua Dkt. Mabiki.
Kwa upande
wake Mratibu wa tiba asili na tiba mbadala mkoa wa Morogoro Dkt. Wille –Anne
Ngalula alisema kuwa jukwaa la ubunifu la tiba asili Tanzania lililoanzishwa na SUA linaendeleza
malengo na jitihada za Serikali katika swala zima la utoaji wa dawa na
kuboresha afya nchini kupitia tiba asili.
’’Kwa sasa
Mkoa wa Morogoro una waganga wa tiba asili waliosajiliwa na Baraza la Tiba Asili Tanzania wamefikia 1872 na tayari
maduka 71 ya tiba asili yamesajili katika mkoa wa Morogoro, hii inaonyesha
muamko mkubwa uliopo kwa wganga hawa katika kufuata sharia na kanuni za
serikali katika utoaji wao wa huduma lakini pia muitikio wa wananchi katika
kutafuta huduma zao ndio maana wanaongezeka siku hadi siku nah ii inatokana na
kazi kubwa iliyofanywa na SUA pamoja na timu yetu ya mkoa na ’’´alieleza Dkt.
Ngalula.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyamna vya Waganga wa Tiba Asili Tanzania Mkoa wa
Morogoro (SHIVYATIATA) Ramadhani Sanze ameishukuru SUA kwa kuendelea kuwa
mlezi wa waganga wa tiba asili nchini na kwa jitihada wanazifanya katika
kuboresha utoaji wao wa huduma kwa wagonjwa kwani imeongeza thamani ya dawa zao
lakini pia kuwajengea kuaminika na kujiamini katika utoaji wa huduma na hivyo
kuwaongezea elimu na kipato.
Maadhimisho ya tiba ya wiki ya tiba asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki yamefanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za ugani kwa waganga wa tiba asili kwenye maeneo yao ya kutolea huduma,kongamano la kisayansi la tiba asili kwa njia ya mtandao pamoja na maonesho makubwa ya kanda ya mashariki yaliyokutanisha waganga wa tiba asili na wadau wengine kwenye mnyororo wa thamani wa tiba asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.