Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUNDU LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI YA UCHOCHEZI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao (Chadema) Tanzania Bara, Tundu Lissu na wenzake wanne.
Ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh

Washtakiwa hao kwa pamoja Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com