Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege akifungua Kikao kazi cha wadau wa ushirika kutoka Mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika leo September 10,2021 jijini Dodoma.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege,akisisitiza jambo wakati wa Kikao kazi cha wadau wa ushirika kutoka Mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika leo September 10,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege (hayupo pichani) wakati wa Kikao kazi cha wadau wa ushirika kutoka Mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika leo September 10,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,Theresia Chitumbi,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Kikao kazi cha wadau wa ushirika kutoka Mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika leo September 10,2021 jijini Dodoma.
.....................................................................
Na Alex Sonna,Dodoma
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege amevitaka vyama vya ushirika nchini, kujiendesha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na ushirika wenye kugusa makundi yote,vijana,wazee kina mama na wafanyakazi wa makundi yote.
Pia,amesema wanaenda kuanza kutumia mifumo ya Kieletroniki katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ambazo zitawasaidia kujiendesha kisasa.
Hayo ameyasema leo Septemba 10,2021 jijini Dodoma wakati wa Kikao kazi cha wadau wa ushirika kutoka Mikoa mbalimbali nchini,Dkt.Ndiege amesema kwa sasa ni lazima kuwe na ushirika wa kisasa na kuachana na yale mazoea.
“Lazima tubadilike tuwe na ushirika ambao unawagusa vijana,wazee kina mama na wafanyakazi na makundi yote wavuvi watu wa habari lazima tusibaki na ushirika wa kizamani hata mifumo yetu lazima iende kisasa.Wewe kama unaendelea kutembelea na makaratasi wenzako wapo kwenye simu wanapata information lazima na sisi tuendane na hali halisi ya nchi yetu jinsi ilivyo,”amesema.Dkt.Ndiege
Aidha,Dkt.Ndiege amesema ili ushirika uweze kwenda vizuri ni lazima kuwe na imani kwa kile ambacho kinafanyika ambapo watu wasipokuwa na imani ni sawa na kazi bure.
“Kwa sasa tunachotamani kwa ukubwa ni imani katika vyama vya ushirika watu wasipokuwa na imani hata tupige kelele au tuweke mifumo gani hawatatumia fursa hizo.Unaweza ukaenda kijijini ukapiga shule yako wanakusikiliza wanakwambia miaka kumi chama chetu kilikuwa kinaleta pembejeo lakini sasa hivi hakuna.
“Hatuwezi kwenda bila kuleta imani hili ni jukumu letu sote lazima tuanze kwa kujenga imani kwa kuwa waaminifu,”amesema.Dkt.Ndiege
Amesema malengo yao ni kuhakikisha kunakuwa na vyama imara vya ushirika ikiwemo kuviona vyama hivyo vinakuwa na mifuko ya pembejeo ili viweze kujitegemea.
“Ni bora kuwa na vyama vichache na sisi tunajikita na kuwa na vyama imara vya ushirika kwa sababu hiyo tunayo malengo ambayo yatatuisaidia mojawapo kwenye vile vyama vya mazao tungependa kuona vyama hivyo vinakuwa na mifuko ya pembejeo na sisi tutajenga mazingira jambo hili liende vizuri,”amesema Dkt.Ndiege
Vilevile, amesema lazima waanze kutoa huduma mbalimbali kwa wanaushirika ikiwemo huduma ya Bima ya afya ili wanachama waone umuhimu wa kuwa katika vyama hivyo.
“Tunataka kuona vyama vya ushirika vikitumia mifumo ya masoko ni namna gani ya kumsaidia mkulima kuweza kupata soko ,Tume ya Ushirika ipo tayari kushirikiana na wadau kuhakikisha wanapata masoko,”amesema Dkt.Ndiege
Pia,Dkt.Ndiege amesema kuna changamoto ya wizi katika vyama vya ushirika hivyo wamejipanga kwa miaka mitano ijayo kuwashughulikia wote ambao wataiba katika ushirika.
“Tumejikita zaidi kuingia katika mifumo ya kieletroniki katika vyama vya ushirika na tayari zoezi hili limeanza na tutatunza taarifa vizuri na tunawaalika wadau kulibadilisha hili.Tunataka mifumo yote wameingia wa wanachama wangapi na amepata pembejeo kiasi gani,” amesema.
Pia,vyama vya ushirika kuanzisha na kusimamia viwanda vikubwa na vidogo lengo likiwa ni kuongeza thamani za mazao nchini.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,Theresia Chitumbi amesema Mkutano huo upo kwa ajili ya kuaandaa ushirika mpya ambao utaenda kisasa.
“Tupo hapa kuaandaa mikakati ya Tume ya Ushirika kwani ni wadau wa ushirika tupo kwa ajili ya kuleta ushirika mpya na hilo ndio lengo la Rais wetu na tumeona Nchi nyingi ambazo ushirika umesimama ndio wana maendeleo makubwa,”amesema
Amesema ushirika wa zamani ulikuwa wa mazao tu lakini sasa hivi wamejipanga kuwavuta vijana na kuubadilisha ushirika na uwe wa kidigitali.
“Mimi kwa mtazamo wangu tunatakiwa kubadilika tuwe na ushirika wa kidigitali kuliko kwenye makatarasi ukiwa kidigitali kila kitu kinaonekana tumeanza kuwaingiza vijana kwa kufanya mashindano ya insha na wameanza kuujua ushirika ni nini,”amesema.
Social Plugin