Waandishi wa habari mkoani Geita, Consolata Evarist wa Global TV, Esther Sumira wa Azam TV na Muta Robert wa Majira, wamenusurika kifo katika ajali baada ya gari aina ya Pajero Mitsubish waliyokuwa wanatumia kuacha njia na kuanguka.
Consolata na wenzake walikuwa wanaelekea Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kutafuta habari ambapo walipata ajali hiyo wakiwa hawajafika safari yao.
Hata hivyo waandishi hao wa habari wamesema wanamshukuru Mungu kwani licha ya gari walioyokuwa wakitumia kuanguka lakini wao wametoka salama zaidi wamepata maumivu madogo madogo na baada ya kutoka salama, taratibu za kipolisi zimefanyika na wao kuweza kuendelea na majukumu yao ya kazi.
Social Plugin