ASKARI WALIOMUUA HAMZA WAPEWA ZAWADI


JESHI la Polisi nchini limewapa zawadi askari walipambana na kumuua mtu mmoja aliyefahaika kwa jina la Hamza Mohammed mkazi wa Upanga, Dar es Salaam aliyejihami kwa silaha na kuua askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa Kampuni ya SGA.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Septemba 20, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akizungumzia tukio hilo lililotokea Agosti 25, 2021 katika jirani na ulipo Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam.

“Askari hawa (Waliopambana na Hamza) miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa.

“Askari Polisi walipambana kuhakikisha kwamba madhara makubwa zaidi ya yale yaliyotokea hayatokei, nani ambaye hafahamu kama yule mhalifu angeondoka na zile silaha zilizokuwa na magazine 2 na risasi 60 na zingine alizokuwa nazo nini kingefanyika.

“Kama risasi zingepigwa ovyo ovyo na Askari walioenda kupambana pale na jinsi mlivyoona tabia ya wananchi wakisikia matukio wanavyojirundika ni dhahiri kungekuwa na vifo vya wananchi wasiokuwa na hatia.

“Mtu yeyote mwenye taarifa za kweli za majambazi wanaofanya unyang’anyi wa kutumia silaha na taarifa hizo ziwezeshe kukamatwa kwa mhalifu akiwa na silaha ile, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM, litatoa milioni 2 kwa mtoa taarifa na litatunza siri,” Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post