Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi akionesha ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu
*******
Katika kuhakikisha wakulima wazao la
dengu katika halimashauri ya wilaya ya Shinyanga hawapunjwi na wafanyabiashara,
Wakala wa Vipimo mkoani Shinyanga (WMA),
wameendelea kufanya ukaguzi wa mizani zinazotumika sehemu tofauti hasa kwa wanunuzi
wa zao la dengu na kufanikiwa kukamata vipimo feki vinavyotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara
wasiokuwa waadilifu kununua zao hilo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo
(WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi amesema lengo la kufanya ukaguzi
huo ni kutaka kubaini mizani zisizo na viwango ambazo hazitoi kipimo
kinachostahili.
Mahundi amesema katika kuhakikisha wakulima wanauza
mazao yao kwa kutumia mizani sahihi iliyohakikiwa na wakala hao wameweka
utaratibu wakutoa elimu kwa wananchi pamoja na kufanya ukaguzi wakushtukiza ili
kubaini wale wote wanao vunja sheria ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi
yao.
“Nawapongeza
wakulima wa zao la dengu katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga maana kwa
sasa baada ya kupata elimu wamekuwa wakitoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa
wafanyabishara wasiokuwa waadilifu wanaotumia ndoo zilizotanuliwa na moto kwa
ajili ya kuwaibia wakulima,”amesema Mahundi.
Ameeleza kuwa, kwa Mujibu wa
Sheria ya Vipimo Sura 340, Wakala wa Vipimo ndiyo wenye jukumu la kusimamia
usahihi wa vipimo vinavyotumika au vinavyotarajiwa kutumika kufanyia biashara
kwa lengo la kumlinda muuzaji na mnunuzi.
Ameeleza kuwa kwa mtu yeyote
atakayebainika akitumia vipimo visivyo sahihi kumuibia mkulima faini yake ni
kuanzia shilingi laki 1 mpaka milioni 10.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi akionesha ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi akionesha ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu
Ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com