Mwalimu Neema Kanyonyi ambaye ni Mwalimu wa wanafunzi wasiosikia katika shule inayotoa elimu maalumu Turwa iliyopo mjini Tarime Mkoani
Mwalimu Mekaus Maingu ambaye ni Mlemavu na Mwalimu wa wanafunzi wasiosikia shule ya msingi Turwa.
Mkuu wa kitengo katika shule ya Turwa Mwl:Magutu Philipo
***
Na Frankius Cleophace Tarime
Watoto wenye umri kati ya miaka sifuri mpaka mitano katika shule ya Msingi Turwa Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara inayotoa elimu maalumu bado wanakabiliwa na changamoto ya Lugha za alama ambazo zinatambulika na serikali hivyo wazazi na walezi wameaswa kuendelea kuwajengea misingi bora waoto wenye ulemavu.
Hayo yamebainishwa na Neema Kanyonyi ambaye ni Mwalimu wa wanafunzi wasiosikia katika shule inayotoa elimu maalumu Turwa iliyopo mjini Tarime Mkoani Mara akizungumzia siku ya Lugha ya alama kimataifa ambayo ufanyika kila mwaka septemba 23.
Mwalimu Neena alisema kuwa changamoto wanayokumbana nayo kwa watoto hususani wenye umri mdogo chini ya miaka mitano ambao wengi wao ni darasa la awali hawajui Lugha za alama ambazo zinatambulika na serikali jambo ambalo linawachukua muda katika ufundishaji.
“Watoto wengi wenye ulemavu wa kusikia wanapokuwa nyumbani wanafundishwa alama tofauti na alama za kitalaamu jambo ambalo linatupa changamoto katika ufindishaji hivyo nawasisitiza wazazi na walezi kuleta mapema watoto wao shuleni” alisema Neema.
Vilevile Neema aliongeza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya mabweni pamoja na vifaa vya ufundishaji vikiwemo vitabu nakuomba serikali kusaidia suala hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo katika shule ya Turwa Mwl. Magutu Philipo aliongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni hukosefu pia wa kifaa cha kupimia walemavu wenye usikivu.
“Tunashukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya elimu katuka shule yetu maalumu ya Turwa lakini bado kunachangamoto mbalimbali kama nilivyosema hicho kifaa cha kupimia welemavu wa kuisikia hautuna shuleni hapa tunaomba serikali pamoja na wadau watusaidie kutatua chanagamoto” hiyo, alisema Magutu.
Vilevile Mekaus Maingu ambaye ni Mlemavu na Mwalimu wa wanafunzi wasiosikia alisisitiza wazazi na walezi kupeleka watoto wenye ulemavu shuleni ili waweze kupatiwa elimu kama watoto wengine huku akibainisha kuwa pia kuna changamoto ya vitabu vya Nukta Nundu.
“Tunawanafunzi wenye ulemavu wa kutoona lakini hakuna kitabu cha Nukata nundu hata kimoja ni changamoto kubwa kwangu mimi kama mwalimu licha ya miundombinu ya shule kuwa mizuri lazima na vifaa vya kujifunza na ufundishaji viwepo”, alisema Maingu.
Wazazi na walezi waone umhimu wa kuwapeleka watoto wote shule ili kupatiwa elimu nakuondokana dhana potofu yala kuficha majumbani watoto wenye ulemavu kwani kila mtoto ana haki ya kupata elimu,hususani watoto kuanzia miaka sifuri mpaka nane wanapaswa kijengewa misingi bora.
Vilevile suala la malezi na makuzi ni jukumu la wazazi wote na jamii kwa ujumla tuungane kwa pamoja kuhakikisha watoto ambao ni tunu ya taiifa wanapatia haki zao za msingi ikiwemo pia mavazi.