WAZIRI BITEKO: MICHEZO NI AFYA TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA

 

Mshindi wa kwanza timu ya wanaume kukimbia mita 100 kutoka Wizara ya Madini David Ibrahim akipewa medali ya dhahabu na Waziri wa Madini, Doto Biteko katika Bonanza yaliyofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya  Madini Prof. Idris Kikula (kulia) wakiwa kwenye mazoezi ya kuzunguka uwanja katika Bonanza la Wizara na Tume ya Madini lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Doto Biteko akitoa medali ya dhahabu kwa Mshindi wa kwanza timu ya wanawake kukimbia mita 100 kutoka Wizara ya Madini Bi. Hilda Masanche katika Bonanza la Wizara na Tume ya Madini lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba akipewa medali ya fedha ya kuwa mshindi wa pili wa kukimbia na yai katika Bonanza la Wizara na Tume ya Madini lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Doto Biteko akitoa kikombe kwa mchezaji bora wa mpira wa miguu kutoka timu ya Wizara ya Madini Bw. Casmiri Daudi katika Bonanza la Wizara na Tume ya Madini lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.
Washindi wa kuvuta kamba timu ya wanawake kutoka Tume ya Madini wakishangilia baada ya kupewa kikombe cha ushindi na Waziri wa Madini, Doto Biteko katika Bonanza la Wizara na Tume ya Madini lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.

 Waziri Biteko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Bonanza kutoka Wizara na Tume ya Madini katika Bonanza hilo  lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.



IMEELEZWA  kuwa, michezo inaleta afya, akili , urafiki na kuwaweka pamoja Wafanyakazi wa Wizara pamoja  na Taasisi zake.

Hayo yamebainisha leo Septemba 11, 2021 na Waziri wa Madini, Doto Biteko wakati wa ufunguzi wa Bonanza ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini lililofanyika katika Viwanja vya Kilimani, Jijini Dodoma.

“Nawapongeza Wafanyakazi wote kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali , tuendelee kufanya mazoezi ili tuweze kupata nguvu ya kuendelea kufanya kazi ya kulinda rasilimali zetu na kukuza Uchumi wa Nchi,” amesema Waziri Biteko.

“Nimechezesha vizuri mechi ya mpira wa miguu kama refa bila upendeleo wowote , niendele kuwapongeza wachezaji kwa kuwa mahiri na kucheza vizuri,” ameongeza Waziri Biteko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewapongeza washiriki wa Bonanza na kuwataka waendelee kufanya mazoezi mara kwa mara maana michezo ni furaha.

Naye, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, anawasisitiza watu wafanyemazoezi  kwa kuwa ni moja kati ya kinga ya kuufanya mwili kuwa imara ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

“Msisitizo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ni kwamba Wizara na Taasisi  zote za Serikali zifanye mazoezi kwa pamoja, na mazoezi hayo ni maandalizi ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambayo yamerudishwa na Serikali,”amesema Mhandisi Samamba ”.

Kwa upande wake, Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Ruben amesema kuwa watu wapo ofisini lakin ukija kwenye mazoezi wapo, rai yangu tusiache mazoezi tushirikiane na kuwa pamoja Wizara na Tume ya Madini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post