Vigogo,Yanga SC wamechapwa 1-0 na wenyeji Rivers United, katika mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.
Yanga wanaaga mashindano hayo kwa kichapo cha jumla cha 2-0 kufuatia kuchapwa 1-0 Jumapili iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi hao wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa, Yanga jitihada zao za kupindua meza kimataifa zimekwama nchini Nigeria kwa kuwa wamefungwa tena.
Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi wa zaidi ya bao 1-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Leo pia ugenini nchini Nigeria Yanga imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao 2-0.
Safari yao na malengo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika imeyeyuka mazima hivyo wanarudi Dar es Salaam.
Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamefanyiwa vitendo vya kihuni na wapinzani wao hasa kwenye suala la vipimo vya Corona.
"Tumefanyiwa mambo ya kihuni na tumepewa matokeo ya Corona dakika 45 kabla ya mchezo huu ni uhuni,".
Social Plugin