SPIKA JOB NDUGAI KESHO KUZINDUA WIKI YA ASASI ZA KIRAIA 'AZAKI' DODOMA...ZAIDI YA ASASI 150 KUSHIRIKI MAONESHO

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Blind Mission (CBM)Nesia Mahenge akiongea na Waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya wiki ya AZAKI yanayoanza kesho Jijini Dodoma.

***
Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 blog DODOMA.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kesho anatarajia kufungua wiki ya Asasi za Kiraia(AZAKI) ambapo jumla ya Asasi zaidi ya 150 zitashiriki katika maonyesho  lengo likiwa ni kuonesha mchango wake katika maendeleo ya Taifa.

Hayo yameelezwa mapema leo Jijini Dodoma  na Mkurugenzi Mkazi wa Christian Blind Mission (CBM)  Nesia Mahenge wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu kuelekea wiki ya AZAKI na kusema itaanza na matembezi ya amani yatakayoanza saa moja asubuhi kuanzia shule ya sekondari Dodoma hadi uwanja wa Jakaya Kikwete.

Bi. Mahenge amesema pamoja na mambo mengine wiki hii inawaleta wadau mbalimbali wa Maendeleo nchini ikiwemo Wananchi,Serikali,AZAKI na sekta binafsi  ambao wote kwa pamoja watajadili na kusherehekea mchango wa AZAKI katika kuleta maendeleo nchini.

"Tunawaita wadau mbalimbali wa maendeleo kujumuika nasi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo   ushauri wa kisheria,kufahamu kazi tunazofanya na kusherehekea kwa pamoja ,"amesema.

Licha ya hayo Mahenge ameeleza kuwa uzinduzi huo wa wiki ya AZAKI utahudhiriwa na wahisani wa maendeleo wakiwemo ubalozi wa Denmark Utakaowakilishwa na Sascha Mulla na Ubalozi wa Canada utawakikishwa na Ms.Helen Fytche.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa United Nations Association (UNA) Reynald Maeda amewataja Viongozi na wageni mbalimbali kutoka Serikalini watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe na mwakili kutoka Wizara ya Afya Vickness Mayao.

"Katika kusherehekea mafanikio  ya sekta ya AZAKI na ubia Wetu baina ya wananchi maonesho yatakayofanyika tarehe 23 Hadi 24 Oktoba Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na kutakiwa na burudani kutoka Kwa wasanii mbalimbali kama Profesa Jay,Sheta,Barnabas,Gnako,na wasanii wa Dodoma,"amesema.

Ameeleza kuwa wiki ya AZAKI hukutanisha wadau wa maendeleo kujadili masuala ya masingi kuhusu ustawi wa sekta pamoja na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Aidha amefafanua kuwa maendeleo yanayoletwa na AZAKI si maendeleo ya kifedha tu bali katika maeneo mengine ikiwemo maendeleo ya wanachi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo kuongeza ushirikishwaji wa watu wote kwenye jamii,kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na Watoto pamoja na kuongeza nguvu katika ufuatikiaji wa rasilimali za umma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post