Mrembo mmoja amelalamika kuwa barabara mbovu inayounganisha jamii kadhaa katika eneo lake imemzuia kupata mume.
Kulingana na dada huyo, wanaume ambao wanatakiwa kuoa watu sampuli yake, huvamiwa kila wakati na watu wapya hawawezi kuingia katika jamii yake sababu ya barabara mbovu.
Tovuti ya habari ya Nigeria, Legit.ng ilipakia maoni ya wanamitandao kuhusu malalamishi ya mrembo huyo Kipusa mrembo nchini Ghana amelalamikia namna anahangaika kupata mume sababu ya barabara mbovu inayounganisha jamii katika eneo lake.
Katika video ambayo imewavunja mbavu wanamitandao, mrembo huyo alihoji kuwa wakati mwingine wageni wanapoingia katika mji wake na kutaka kutumia barabara yao, huwa wanakata tamaa na kurudi walikotoka.
Isitoshe, dada huyo ambaye hakujitambulisha wala jamii yake, alidai kuwa visa vya wizi wa kimabavu vimekithiri sana eneo hilo na kuibia wanaume mali ambayo wangelitumia kuoa watu sampuli yake.
"Jinsi barabara ilivyo mbovu, majambazi wanaendelea kuwaibia wanaume ambao wangetaka kutuoa. Hivyo tunaiomba serikali ije kututengenezea barabara ili tupate mapenzi," aliongeza.
Maoni ya wanamtandao
Priscilla Vidza alisema: "Dereva mmoja wa teksi aliniambia angelikuwa ni mpenzi wangu angeachana nami kwa sababu ya hali mbaya ya barabara yangu oo."
Fx Amoah alihoji: "Nyinyi nyote kuamka alfajiri kupanga misururu mirefu ya kuwapigia kura wanasiasa na kushangilia mtaani wakati mwakilishi wa chama chenu anaposhinda bila kujali anafanya kazi hiyo au anahitaji ofisi tu kwa ubadhirifu wa fedha."
Asiedu Lawrencia: "Inaweza kuwaukweli kwa sababu niliwahi kumuona bi wa mjini na baba yangu akiuliza kama atakuja hapa barabara ya kuelekea mjini hmmmm bado nawaza jibu naenda kumpa."
Nutsu GH alisema: "Eric Abaidoo nadhani itakuwa fursa nzuri ya utafiti kuchunguza athari za barabara mbaya kwenye matokeo ya baadaye ya ndoa ya wanawake katika jamii hii."
Chanzo - Tuko News
Social Plugin