Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (aliyevaa tai) akiongoza zoezi la kukata keki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB tawi la Shinyanga imezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kukata na kula keki na wateja na wafanyakazi wake huku ikiahidi kuboresha zaidi huduma zake ikiwa ni chaguo la kwanza kwa huduma za kibenki ikijinadi katika Nguvu ya Huduma 'Power of Service'.
Akizungumza mapema leo Jumatatu Oktoba 4,2021 wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amewashukuru wateja kuendelea kuiamini na kutumia huduma Benki ya CRDB.
“Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika kila mwaka kuanzia Oktoba 4. Sisi Benki ya CRDB tunaitumia wiki hii kutafakari juu ya huduma tunazotoa, kusikiliza wateja na wadau mbalimbali wapi tuboreshe. Kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja ni The Power of Service (Nguvu ya huduma)”,amesema Wagana.
Aidha amewashukuru wateja kwa kuichagua na kuipenda Benki ya CRDB na kupata huduma kama chaguo lao huku akiwaomba kuwa Mabalozi kwa kupeleka wateja wapya katika Benki hiyo.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney amesema wataendelea kutoa huduma nzuri na bora ili kuhakikisha Benki ya CRDB inakuwa chaguo la kwanza la wateja katika huduma za kibenki.
“Kupitia kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja mwaka 2021 ya ‘Nguvu ya Huduma’ tutawezesha wafanyakazi wetu na wadau wote kuhakikisha huduma zetu zinakuwa bora wakati wote na litakuwa chaguo la kwanza katika huduma za Kibenki”,amesema Mneney.
“Tunawashukuru wafanyakazi wetu kwa huduma wanazotoa ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora. Tunawashukuru pia wadau wote wanaohakikisha huduma bora kwa wateja zinatolewa sambamba na Wanahisa, Bodi ya CRDB na watoa huduma wote na wadau wote”,ameongeza.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa tatu kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Keki Maalumu kwa ajili ya Wateja na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (katikati) akizungumza wakati wa zoezi la kukata keki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa zoezi la kukata keki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (aliyevaa tai) akiongoza zoezi la kukata keki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB ,MC Mama Sabuni akifungua Shampeni wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimpatia kinywaji mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (aliyevaa suti) akigonga Cheers na wateja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akiwashukuru wateja wa Benki ya CRDB kwa kuendelea kutumia huduma za Benki hiyo.
Wateja wa Benki ya CRDB wakiendelea kupata huduma wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakicheza muziki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakicheza muziki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Burudani ya muziki ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Wateja na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakicheza muziki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Jumatatu Oktoba 4,2021 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin