Gari aina ya Toyota Landcruiser Prado limetumbukia katika Bahari ya Hindi eneo la ufukwe wa Coco Jijini Dar es saalaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Oktoba 5,2021 na kwamba hakuna madhara yoyote yaliyotokana na ajali hiyo baada ya dereva wa gari hilo kuokolewa.
Amesema wanasubiri afya yake iimarike ili wafanye uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa dalili zinaonyesha alikuwa ni mtu mwenye mawazo au tatizo la akili.
"Kule alipokuwa anakwenda kulikuwa hakuna barabara, kama mtu ni mzima huwezi kuona gari linakwenda baharini na wewe ukazidi kukanyaga mafuta",amesema Kingai.
Social Plugin